SALAMU ZA RAMBIRAMBI

SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Uongozi wa Klabu ya waandishi wa Habari Pemba (Pemba Press Club – PPC) tunatoa salamu za rambirambi kwa familia ya  mjane wa Hayati, Rais Magufuli, Mama Janeth Magufuli, watoto, ndugu na jamaa kwa  kuondokewa na mpendwa wao na wananchi wote wa Tanzania kwa pigo hili kubwa.

Ni msiba mzito ambao hatukutarajia, sote tunafahamu jinsi Hayati, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alivyoipenda nchi, alivyowapenda Watanzania na kujitoa kwa watu wake kwa dhamira ya dhati na nia njema ya kuibadilisha taswira ya nchi yake.

“Tumepoteza kiongozi shupavu, madhubuti, mwenye maono, mpenda maendeleo, mwana mwema wa Bara la Afrika na mwanamapinduzi wa kweli, Mhe. Magufuli alikuwa chachu ya maendeleo kwa nchi yetu na Africa kwa ujumla”