Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kiwani katika Wilaya ya Mkoani ndugu Rashid Abdalla Rashid amewataka wananchi wa Jimbo hilo kumchagua na kuendelea kukipigia kura Chama cha Mapinduzi ili kiweze kuwaletea maendeleo wazanzibar na Watanzania kwa ujumla.
Ndugu Rashid ameyasema hayo huko Mwambe wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi katika jimbo la Kiwani.
Amesema katika uongozi wa awamu ya saba inayomalizia kuna miradi mingi ya maendeleo imeekezwa kwa ajili ya kuwaondoshea kero wananchi hivyo ni vyema kuendelea kukiweka madarakani chama cha mapinduzi ili wananchi wazidi kunufaika na maendeleo hayo.
Naye mgombea wa uwakilishi wa jimbo la Kiwani ndugu Mussa Foum Mussa amesema katika kipindi kilichopita wakati akiwa mwakilishi wa jimbo hilo alifanikiwa kusimamia upatiukanaji wa huduma zote muhimu za kijamii ndani ya jimbo hilo hivyo amewataka wanaccm na wapenda amani wote kuwachagua wagombea hao ili kukamilisha yale waliyoyanza.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM Mkoa, Mh Hemed Suleiman Abdalla amewasisitiza wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu kabla na baada ya uchaguzi huku akiwataka wananchi kuondoa hofu kwani serikali iko makini kufuatilia matendo yote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani.
Angalia Video.