Sunday, November 24

Wanahabari watakiwa kuandika taarifa zinazohusiana na hifadhi , utalii na mazingira.

TAKRIBAN hekta Milioni 12 ya misitu katika eneo la Kitropiki ya Dunia limepotea kwa moto mwaka 2018, naweza kusema sawa na kupotea viwanja 30 vya mpira wa miguu kwa dakika.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Global Forest watch ikionyesha kupungua kwa misitu mwaka 2016 na 2017, licha ya upoteaji huo ulianza tokea mwaka 2001.

Kama tunavyojua miti katika eneo hili ni muhimu kwa makaazi ya watu, kutoka makabila mbali mbali ya utoaji wa chakula, miti katika eneo hili muhimu duniani katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

 

Mamilioni ya hekta za misitu imekuwa ikipotea katika karne za hivi karibuni, kutokana na shughuli za kibiashara na kilimo,

Takwimu za mwaka 2018 zinaonyesha kuna utofauti katika upungufu mkubwa wa misitu kwa miaka miwili iliyopita, miti mingi imepotea kutokana na moto.

 

Chama cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania (JET) kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la Marekani(USAID-Protect), chini ya mradi unaolenga kutoa elimu ya kutokomeza ukatili na ujangili kwa wanyamapori nchini, JET kuwa mstari wa mbele kutetea masuala yote ya uhifadhi wa wanyamapori na umuhimu wa kulinda bayonuai zake ikiwemo miti.

Kwa kuona hivo JET iliwafunda waandishi 30 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania bara na Zanzibar, juu ya uhifadhi, uwindaji haramu wa wanyamapori na usafirishaji nchini.

Afisa mwandamizi kutoka taasisi ya kuzuwia na kupambana na Rushwa Tanzania, Ally Katonya amesema waandishi wa habari wanapaswa kujikita zaidi, katika masuala ya wanyamapori na kutokusahau misitu, kuwa ndio chanzo kikubwa cha uingizaji wa fedha nchini.

Serikali iliweza kutaifisha mali zenye thamani ya shilingi Bilioni 4.7, zinazotokana na mazazo ya misitu ni wazi kwamba misitu ni moja ya rasilimali muhimu katika suala zima la uhifadhi wa wanyamapori.

Mazao ya misitu ni muhimu kwa serikali katika mapato, utunzaji wa mazingira na utunzani wa wanyamapori na kuinua sekta nzima ya Utalii, kwani misitu ni kitu muhimu sana katika sekta ya Utalii na wanyamapori nchini.

“Hekta 81 za mazao mbali mbali ya mkurunge yalikamtwa na kuwasilishwa serikalini, tizama mazao hayo yalivyoteketea ni wazi kwamba miti iliteketea kwa wingi, hata hii utakataji wa miti na upigaji wa mkaa ni tatizo pia”amesema.

“Misitu ni moja ya rasilimali muhimu sana inayoingiza fedha nyingi, bado watanzania tumeisahau sekta hiyo na nisekta inayopaswa kulindwa na kuhifadhiwa”amefahamisha.

Afisa kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Salimu Hakim Msemo, amesema makosa ya ujangili ni miongoni mwa makosa, yanapelekea utakatishaji wa fedha na sheria zipo zinatumika pale watuhumiwa wanapotiwa hatiani.

Anasema kuwepo kwa sheria na watuhumiwa kuwatia hatiani na waandishi wa habari kuandika habari hizo, kumepelekea kupungua kwa masuala ya ujangili nchini, ikiwemo kesi ya malkia wa Tembo ambayo iligonga sana katika vyombo vya habari.

Alizitaja baadhi ya sheria hizo kuwa ni, sheria ya uhifadhi wa wanyamapori, sheria ya misitu, sheria ya hifadhi za taifa, sheria mahususi inayohusika na eneo la ngorongoro na sheria ya mazingira, sheria ya utakatishaji wa fedha.

Sheria nyengine ni kanuni na makosa ya adhabu, sheria ya uhujumu uchumi na makosa ya kupangwa yanayoendana na mambo ya ujangili, sheria ya makosa ya adhabu.

Amesema baada ya watuhumiwa kukamatwa na kutiwa hatiani, kumekua na adhabu mbali mbali pamoja na vifungo na faini, pamoja na kutaifisha mali za watuhumiwa hao, ikiwemo mali zilizotumika kusafirisha na nyaraka hizo haramu.

“Hizi sheria ni kali sana sasa zimeanza kutumika na watuhumiwa kutiwa hatiani, hapa ndipo matukio ya ujangili wa wanyamapori yalipoanza kupungua, itafika wakati matukio yataondoka kabisa”amesema.

Mwenyekiti wa chombo cha pamoja National Taksi Fosi Tanzania(NRT) Roberti Mande, amesema mausala ya ujangili wakati mwengine yawiyana na makosa ya kupangwa na yanahusisha watu wengi, wapo ndani ya nchi na nje ya nchi.

Tokea mwaka 2016 National Task Force Anti-poaching (NTAP) ilipoanza, wakati ambao matatizo ya ujangili yalikuwepo na kupelekea zaidi ya 60% ya wanyama kupotea, zaidi ya Tembo 43000 waliuwawa kati ya miaka 2010 hadi 2014.

Bandari ya Dar na Zanzibar ndizo zilizokuwa zikitumika sana kusafirishia biashara hiyo, ambapo mwaka 2009-2013 zaidi ya tani 45000 za ndovu zilizosafirishwa ulimwenguni kote kutoka Tanzania.

Mwaka 2013 Tanzania iliyoorodheshwa katika nchi nane ambazo wanyama walishafirishwa nje ya nchi na serikali kuandaa Operesheni Tokomeza, mwaka 2014 Tanzania ikandaa mkakati wa kitaifa wa Kupinga ujangili,

“Uhalifu unafanyika kimtandao, yapo maeneo kwenye uhifadhi uhalifu unafanyika, pia katika maeneo ya mjini lazima kuwe na mtandao mkubwa wa kuzuwia uhalifu”amesema.

Kutokana  na mikakati hiyo mwaka 2015 hadi 2020, waliweza kubaini watuhumiwa zaidi ya 3,000 wanaohusika na ujangili wawanyama pori, katika operesheni 360 walizozifanya katika nchi mbali mbali ikiwemo Kenya, Mozambiqi, Malawi na Unganda, huku washukiwa 2000 wakitiwa mikononi.

Mande amesema walichunguza takriban visa 300 vya wanyamapori kwa hali ya juu kwa kushirikiana na mataifa, pia waliweza kukamata vipande 14,741 vya pembe za ndovu, pamoja na kushikilia pembe 25 za vifaru na imewakamata zaidi ya wanyamapori wazima 2000, ilibaini zaidi ya bunduki 2000 na risasi 25,000 kukamata na kukamatwa zaidi ya Tania 10,000 za mbao miti.

“Kesi 914 zinazohusiana na wanyamapori zilifikishwa katika mahakama, kesi 691 zilishitakiwa na kutiwa hatiani sawa na asilimia 75%, huku washukiwa 1,600 wamefungwa jela kati ya miaka 10 na 20 na washukiwa 43 walilipa faini karibu shilingi Bilioni 2,”alisema.

Hata hivyo masuala ya ujangili ya wanyamapori yamepungua kwa asilimia 80%, huku ikielezwa kamba idadi ya Tembo imeongezeka katika miaka 2018-2020 na kuleta matumaini makubwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania (JET) John Chikomo, aliwataka waandishi kuwandika habari za usahihii, ikizingatiwa wanyama na mazingira ni rasilimali muhimu.

John amesema mazingira ni kitu muhimu kwa maisha ya binaadamu na viumbe mbali mbali duniani, hivyo ni wakati wakutumia kalamu zao katika kuelimisha jamii.

Mwenyekiti wa JET Dr Ellen Otaru, alisema suala la uhifadhi wa wanyama pori lina uwanja mkubwa sana, kwani hata mazingira na vilivyozunguka vyote vinapaswa kuhifadhiwa.

Email:abdisuleiman33@gmail.com

0718 968 355

MWISHO.