Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ambae pia ni Mwenyeiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa Mh. HEMED SLEIMAN ABDALLA amewataka wananchi kuacha tabia ya kuchukuwa sheria mikononi mwao kwani vitendo hivyo vinaweza kuhatarisha uvunjifu wa amanii nchini.
Mkuu wa Mkoa huyo ametowa wito huo huko ofisini kwake Chake Chake wakati akizungumza na ZBC kufuatia tukio la kijana mmoja kuwapinga mapanga watu watatu huko katika kijiji cha Kangagani Wete.
Amesema katika kipindi hichi cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu kumekuwa na mikusanyiko ya watu mbali mbali hivyo kwa wale ambao watahudhuria katika kampeni hizo hawana budi kuhakikisha wanaendelea kudumisha amani na utulivu kwa usalama wao na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake kamanda wa polisi Mkoa wa Kusini Pemba Msaidizi kamishana wa Polisi MAKARANI KHAMIS AHMED amesema kwa ujumla hali ya Mkoa hadi sasa ni salama na inaendelea kuwa na amani hivyo hakuna budi kwa wananchi kudumisha amani iliyopo.
Amewataka wananchi itakapofikia tarehe 28 kuhakikisha kila mwenye haki ya kupiga kura kwenda kupiga kura kwa amani na jeshi la polisi liko imara katika kuhakikisha hakuna vurugu zozote zitakazo tokea.
Angalia video.