Sunday, November 24

Wagombea CCM Jimbo la Chonga wanadi sera zao.

MENEJA Kampeni za CCM Mkoa wa Kusini Pemba Mohamed Aboud Mohamed, akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la Chonga Juma Mohamed Juma, kwa wananchi na wanaCCM wa jimbo hilo, wakati wauzinduzi wa kampeni za jimbo hilo huko Pujini Wilaya ya Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WAGOMBEA Ubunge na Uwakilishi Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake, kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) wamesema iwapo wananchi watawapa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo, watahakikisha wanashirikiana katika kupeleka maendeleo pamoja na kutatua kero zote zainazowakabili wananchi wa jimbo hilo.

Wagombea hao wamesema kuwa kwa sasa wanasubiri ridhaa za wananchi tu, ili kuanza harakati zakulibadilisha jimbo hilo ambalo kwa miaka mingi lilisahauliwa na viongozi wa jimbo waliokuwepo.

Wakizungumza katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za jimbo hilo, huko katika uwanja wa Mpira wa Skuli ya Pujini Wilaya ya Chake Chake, zikiongozwa na meneja wa Kampeni za CCM Mkoa wa kusini Pemba Mohamed Aboud Mohamed.

MJUMBE wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake, huko katika uwanja wa Pujini.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Juma Mohamed Juma, alisema iwapo atapata ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo aliahidi kushirikiana katika kuleta maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo elimu, afya, barabara, maji na uvuvi.

Naye mgombea uwakilishi jimbo hilo Suleiman Massoud Makame, aliahidi kutataua kero zilizomo ndani ya jimbo hilo, kwa kufuata nyayo za serikali ya awamu ya 7 chini ya Dk Shein, ambao imefanya mambo mengi na makubwa ambayo hayajawaki kutokea.

Kwa upande wake meneja kampeni Mkoa wa kusini Pemba Mohamed Aboud Mohamed, wakati akiwatambulisha wagombea hao na kuwanadi, alisema wagombea hao iwapo watapata ridhaa watahakikisha wanafuata nyayo za mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM kuwa yanayokuja yanafurahisha.

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Yussuf Ali Juma, akimtambulisha meneja kampeni za CCM Mkoa wa Kusini Pemba Mohamed Aboud Mohamed kwa wananchi na wanaCCM, wakati wa Ufunguzi wa Mkapeni za CCM jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

“Wagombea wetu mara hiio wote wanauzika kwa wananchi, Dk.Magufuli amehakikisha uchumi umekuwa na ameijenga Tanzania mpya kwa kuondosha dhulma, ufisadi na majungu”alisema.

Aliwataka wananchi kutokufanya kosa mwaka huu Oktoba 28 itakapofika, kwa hakikisha wanawachagua viongozi wa CCM ili kuwaletea maendeleo.

Akimzungumzia Mgombea Urais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi, amekuja na dhamira ya kubadilisha uchumi na kuleta mabadiliko nchini kwa kuwasaidia wafanyabiasha, wajasiriamali na wanawake.

Aidha aliwataka wananchi wa jimbo la Chonga kutokuwaangusha wagombea wao, ikiwemo urais, ubunge, uwakilishi na udiwani, kwa kuhakikisha wanawachagua kwa kishindo.

Meneja huyo kampeni aliwatahadharisha wanachi kutokukubali kuingizwa katika mambo yanayohatarisha amani ya nchi, kwani vyombo vya ulinzi na usalama vipo tayari katika kulinda amani ya nchi, huku akiwanasihi vijana kutokuingizwa katika matukio hayo.

Naye mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Yussuf Ali Juma, aliwataka wananchi wasikubali kushawishiwa pamoja na kuwaombea kura wagombea wote wa CCM Taifa.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mstaafu Wilaya ya Chake Chake Zainab Khamis Shomar, aliwataka wananchi na wanachama wa CCM kuendelea kuwa wamoja na kuhakikisha CCM inarudi tena madatrakani.

Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, alisema wananchi wa Chonga mwaka huu, wanataka kuushangaza dunia kwa kuhakikisha jimbo hilo linarudi katika mikono ya CCM.

Aidha aliwaomba wananchi kuendeleza kuitunza amani ya nchi hivi sasa na baada ya uchaguzi, huku akiwatadharisha wananchi hususan vijana kutokukubali kushawishiwa kwani vyombo vya sharia viko macho.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chake Chake Khamis Salum, aliwataka wananchi kwenda kupiga kura na baadae kurudia majumbani kwao, badala yake wasubiri kusheherekea ushindi wa CCM.

MENEJA kampenzi za CCM Mkoa wa Kusini Pemba Mohamed Aboud Mohamed, akiwahutubia wananchi na wanaCCM wa Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake, wakati wa Ufunguzi wa Kampeni za chama hicho katika uwanja wa Pujini.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

MENEJA Kampeni za CCM Mkoa wa Kusini Pemba Mohamed Aboud Mohamed, akimtambulisha mgombea Uwakilishi jimbo la Chonga Sulieman Massoud Makame, kwa wananchi na wanaCCM wa jimbo hilo, wakati wauzinduzi wa kampeni za jimbo hilo huko Pujini Wilaya ya Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
VIONGOZI mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba, katikati ni mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Yussuf Ali Juma, akifuatilia mkutano wa uzinduzi wakamopeni za chama hicho katika jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

WALIOKUWA wagombea wa majimbo mbali mbali Mkoa wa Kusini Pemba, wakimsindizika kwa nyimbo “aliyepewa amepewa”mgombea udiwani jimbo la Chonga Time Ramadhan Khati, wakati alipokuwa akitambulisha kwa wanachi na wanaCCM wa jimbo hilo, kwenye uzinduzi wamkutano wa kampeni huko Pujini.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)