MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha NRA Khamis Faki Mgau, amesema iwapo wananchi wa Zanzibar wakachagua kuongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, atahakikisha anapandisha mshara wa walimu kima cha chini kuanzia laki nane (800,000/=), pamoja na vikosi vya SMZ kupokea mshahara sawa na askari wa JWT kwani kazi zao za ulinzi zinafanana.
Mgombea huyo aliyaeleza hayo huko katika uwanja wa kangagani, wakati wa uzinduzi wa kampenzi za chama hicho Kisiwani Pemba, pamoja na kuwanadi wagombea ubunge, uwakilishi na udiwani kupitia NRA.
Alisema mambo hayo yanawezekana iwapo chama hicho kitapatiwa ridhaa ya kuongoza Zanzibar, kwani atahakikisha walimu na vikosi vya ulinzi vinabadilika mishahara yao kutokana na kazi wanazozifanya kwenye nchi.
“Nduguzangu wa kangagani, hii ni fursa yenu pekee adhimu hii ni mara ya kwanza Kangagani kutoa mgombea Urais wa Zanzibar, sasa ni wakati wenu kutumia fursa hiyoo”alisema.
Aidha alisema kuwa NRA inasisitiza suala zima la amani ya nchi ni muhimu, fitna, chokochoko katika kipindi cha uchaguzi hazina nafasi kwa sasa.
Mgombea huo alisema pia chama chake kitakuwa ni muumuni mkubwa wa kuyalinda na kuyatunza Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, pamoja na muumini wa Muungano wa Tanzania na Zanzibar uliopo sasa.
Naye Mgombea Mwenza wa NRA Khamis Ali Hassan, alisema asuala la amani ni muhimu kabla na baada ya Uchaguzi, huku akiwataka wananchi kukichagua chama hicho ili kuleta maendeleo.
Mwenyekiti wa NRA Zanzibar Simai Abrahaman, alisema iwa[po NRA itaongoza nchi basi itaweza kuimarisha uchumi wa nchi, pamoja na kuwaunganisha wanachi wote na kuwa kitu kimoja.
Mgombea uwakilishi jimbo la Ole kupitia NRA Hafidhi Makame Issa, alilaani vikali tukio lililotokea Kangagani la kupigwa mapanga viongozi wa CCM, huku akisema kuwa tukio hilo limeitia doa baya Taifa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.
Katibu wa NRA Mkoa wa Kusini Pemba Khamis Rashid Said, aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kuhubiri suala la amani wanapokuwa katika majukwa, sio kutoa lugha za matusi na kejeli kwa baadhi ya vyama.