Friday, October 18

VIDEO: Wagombea CCM jimbo la Pandani nao wanadi sera zao.

Mjumbe wa Halmashauri kuu  ya CCM Taifa Ramadhan Shaib Juma amewataka wana CCM na wananchi wote wapenda amani kuwachagua wagombea wa Chama cha Mapinduzi na  kujitokeza kuendelea kuomba kura kwa wananchi wote bila ya kujali  itikadi za kisiasa, kwani  sera za CCM zinaelekeza  kuleta maendeleo kwa wananchi wote.

Ndugu Ramadhan amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wana CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Pandani katika Mkutano wa kampeni wa Jimbo hilo huko shengejuu wakati wa kuwanadi wagombea wa nafasi ya Uwakilishi, ubunge pamoja na madiwani.

Kwa upande wake Mgombea wa Uwakilishi wa Jimbo la Pandani ndugu Khamis Dadi Khamis amewaomba wana CCM wote na wapenda maendeleo kumchagua yeye pamoja na wagombea wote wa CCM wa Jimbo hilo ili waweze kuunganisha nguvu zao katika kukuza maendeleo ya Jimbo la Pandani na Zanzibar kwa ujumla.

Amesema CCM ndio chama pekee chenye sera zenye kutekelezeka hivyo kila mmoja anapaswa kukiunga mkono chama hicho huku akiahidi kusimamia kwa karibu harakati za kiuchumi zilizoanzishwa katika jimbo hilo ili kila mmoja anufaike na maendeleo hayo.

Akizungumzia kuhusu changamoto za Vijana kwa upande wa Michezo amesema  watakapo chaguliwa wagombea kupitia Chama cha Mapinduzi  changamoto hizo zitafikia mwisho wake kwani yeye mwenyewe ni mwana michezo hivyo watahakikisha matatizo yote ya kimichezo katika jimbo hilo  yanapatiwa ufumbuzi.

 

VIDEO: