Licha ya juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na Serikali pamoja na Asasi za kiraia kuielimisha Jamii madhara ya Udhalilishaji wa kijinsia kwa Watoto na jinsi ya kutoa ushahidi kwa kesi hizo lakini bado inaonekana matendo hayo yanaendelea kujitokeza kutokana na Muhali uliopo kwa Wanajamii.
Hayo yamesema na wajumbe wa Mtandao wa kupinga Udhalilishaji kutoka Wilaya ya Mkoani katika kikao cha uwasilishaji wa ripoti za utekelezaji wa majukumu yao ya kutoa Elimu juu ya madhara ya Udhalilishaji wa Kijinsia kwa Jamii huko ukumbi wa Chama cha Wandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar [ Tamwma] Mkanjuni Chake chake Pemba. Wanajamii hao.
Wamesema Jamii inaonekana kuyafumbia macho na kuyafanyia suluhu Mitaani matendo ya udhalilishaji jambo ambalo linasababisha kuongezeka sikuhadi siku.
Aidha wameeleza kuwa kuwepo kwa umasikini uliokithiri imedaiwa kuwa ni moja ya sababu inayopelekea kuongezeka kwa udhalilishaji kwa Watoto