Friday, October 18

VIDEO: Mama Maryam Mwinyi amuombea kura DK. Hussein Ali Mwinyi.

 

Waswahili wanasema Mwanamme yeyote Yule ambaye amepiga hatua ya mafanikio basi ujue kuwa nyuma yake kuna mwanamke ambae amesaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kwa upatikanaji wa mafanikio hayo.

Mama  Maryam  Mwinyi Mke wa Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi na yeye kwa upande wake anataka kuthibisha ukweli wa msemo huo kwani wakati wote hatua kwa hatua yuko sambamba na Dr. Hussein Mwinyi katika kuusaka Urais wa Zanzibar kupia tiket ya Chama cha Mapinduzi.

Huko Katika kijiji cha Shumba Mjini Mama Maryam  alikutana na akina mama wa shehia hio ambapo bila ya ajizi aliwaomba akina  mama hao kumchagua Dr. Hussein Ali Mwinyi pamoja na wagombea wengine kupitia chama cha Mapinduzi ili waweze kupata ridhaa ya kuiongoza  Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitanoi jayo kwa lengo la kuendeleza juhudi za Awamu ya Saba ya Serikali ya Mapinduzi ya kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Amesema iwapo watampa ridhaa  Dr. Hussein na Kuwa Rais wa Zanzibar basi atahakikisha anazitatua changamoto zinazowakabili ili wananchi hao waweze kupata maendeleo zaidi.

Hata hivyo akina  mama hao wameahidi kutoa nguvu zao zote katika kuipatia ushindi  CCM.

ANGALIA VIDEO: