Friday, October 18

CHADEMA wafungua kampeni Mtambile.

 

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Saidi Issa Mohamed (kushoto) akimnadi mgombea ubunge wa Mtambile kupitia chama hicho Omar Othaman Nassor, wakati wa uzinduzi wa kampenzi huko kangani sokoni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha Demokrasia Maendeleo Chadema Said Issa Mohamed, amesema iwapo wananchi wa Zanzibar wampatia ridhaa ya kuongoza nchi, atahakikisha anatumia rasilimali ziazopatikana nchini kwa kuipaisha Zanzibar kiuchumi.

Alisema atatumia rasilimali hizo kwa kuunda viwanda mbali mbali ambavyo, vitaweza kuifanya Zanzibar kuzalisha bidhaa ikiwemo mboga mbona na kuuza katika masoko makubwa ulimwenguni.

Mgombea huyo aliyaeleza hayo huko kangani Wilaya ya Mkoani, wakati wa ufunguzi wa kampeni za jimbo la Mtambile na kuwanadi wagombea ubunge na uwakilishi wa jimbo hilo.

Alifahamisha kuwa watahakikisha wanaelimisha vijana kujikita katika kilimo, kwani Zanzibar inauwezo wakuzalisha kwa wingi mchele na kuuzwa kilo shilingi 300.

Alisema iwapo atapata ridhaa hiyo basi ndani ya kiku 100 za uongozi wake, kwani huduma zote zitapatikana bure kutokana na kuwa nyezo za kutoa huduma hizo zipo.

“Sisi tutakapo ingiza madarakani basi huduma zote bure, tukianzia na afya, elimu, maji, tutahakikisha wananchi wanakunywa chai bure asubuhi na usiku kama ilivyokuwa Libya”alisema.

Akizungumzia suala la upandishaji wa mishahara, alisema serikali yake itahakikisha inapandisha mishahara kwa watumishi wote wa serikali, ili kufikia maendeleo yao na kufanya kazi kwa umakini.

Mgombea ubunge wa jimbo la Mtambile kupitia Chadema Omar Othaman Nassor, alisema uwepo wa vyama vingi vya siasa na kila chama kusimamisha wagombea, kunawafanya wananchi kuchagua chama chene sera sahihi ambazo zinaweza kuwapatia maendeleo.

Alisema wananchi wa mtambile kwa muda mrefu walikosa maendeleo, jambo ambalo limemfanya kuwa tauyari kuwatumikia wananchi hao, ili kuwarudishia shukurani zao.

Naye mwakilishiwi wajimbo hilo Haji Kali, alisema matatizo yote ya wananchi wajimbo la mtambile anayatambua hivyo wananchi watarajie makubwa kupitia uongozi wake.