UMASKINI uliokithiri imebainika kuwa ni moja ya sababu inayopelekea Watoto kufanyiwa Udhalilishaji.
Hayo yamesemwa na wdau wa mtandao wa kupinga udhalilishaji kutoka Wilaya ya Mkoani, katika mkutano wa uwasilishaji wa ripoti za utekelezaji wa majukumu yao ya kutoa elimu juu ya madhara ya udhalilishaji wa kijinsia kwa jamii uliofanyika ofisi ya TAMWA Pemba.
Kwa upande wake Shaban Juma Kassim Msaidizi wa sheria kutoka shehia ya Mkanyageni, alifahamisha kuwa udhalilishaji unafanyika zaid kwa watoto wanaokosa malezi ya pamoja ambao wazazi wao wameachana.
Alisema takriban watoto wengi ambao wazazi wao wameachana, wanakosa masomo na badayake wanatumikishwa ili wapate mahitaji yao hali ambayo inaridisha nyuma maendele ya watoto.
‘’Wanawake wengi hususan wanaoishi vijijini ni maskini, hivyo hushindwa kuwalea watoto ipasavyo na kupelekea kudhalilishwa’’,alisema Shaban.
Nae Afisa Tathmini na ufuatiliaji wa chama cha Wandishi wa habari Wanawake Zanzibar Mohamed Khatib Mohamed, amewataka wadau hao waendelee kuzifuatilia kesi, ambazo wameziibua wakati walipokuwa wakitoa elimu.