Thursday, January 16

VIDEO: ADA -TADEA Yazindua Kampeni Mkoa wa kaskazini Pemba.

 

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADA-TADEA  Juma Ali Khatib amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kuiongoza  Zanzibar  kwa miaka mitano ijayo atahakikisha anaifanyia matengenezo makubwa bandari ya wete Pemba kwa lengo kuongeza kipato kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mh, Ali  Juma Khatib ameyasema hayo huko Jadida Wete Pemba wakati alipokuwa akuzungumza na wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho katika uzinduzi wa Kampeni za chama hicho kwa upande wa Mkoa wa kaskazini Pemba.

Amesema bandari ni chanzo kikubwa cha kuingiza mapato na ukizingatia bandari ya Wete ipo karibu na nchi jirani ambazo zinamuingiliano mkubwa na wafanya biashara hivyo atahakikisha anaifanyia matengenezo bandari hiyo.

Mgombea huyo pia amesema chama chake kinaweka mipango mizuri inayotekelezeka kwa ajili ya Vijana kuweza kujiajiri ikiwa ni pamoja na kuwapatia mitaji ambayo itawasaidia katika kuendesha maisha.

Kwa upande wake Mgombea mwenza wa chama hicho kwa upande wa Jamhuri ya muungano Hassan Kijogoo amesema endapo chama chake kitaongoza dola watakahikisha wanasimamia umiliki wa ardhi ili kila mwananchi aweze kufaidika na rasilimali hio.

Angalia video  hii HAPA.