Thursday, January 16

Mgombea Urais NRA:nitauenzi na kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

 

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha NRA Khamis Faki Mgau, amesema iwapo wananchi wakampa ridhaa ya Kuongoza Zanzibar, atahakikisha nauenzi na kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kutokana na kuwa na faida nyingi kwa wazanzibari.

Alisema wananchi wa Zanzibar kwa kiasi kikubwa wanafaida sana na matunda ya Mungano huo, kwani wapo wazanzibari wengi wamekuwa wafanyabiashara wakubwa Tanzania bara, mpaka wengine kumiliki mali kubwa kubwa.

Mgombe ahuyo aliyaeleza hayo huko katika kijiji cha kambini kichokochwe Wilaya ya Wete, wakati wauzinduzi wa mkutano wa jimbo la Kojani.

Alisema chama cha kitahakikisha kinakuwa muumini mkubwa wa Muungano huo uliopo hivi sasa, licha ya baadhi ya vyama kutaka kuuvunja muungano huo.

Akizungumzia suala la Mapinduzi, mgombea huyo alisema atahakikisha chama chake kinatambua umuhimu wa Mapinduzi matukufu ya wanzaniari, kwa kuyaimarisha na kuyaendelea na kuimarika.

“SIsi sera yetu ni kupeleka maendeleo kwa wananchi, tena maendeleo bora na yatakayowaondolea shida wananchi, tukipata serikali tutafaya hayo”alisema.

Alisema watahakikisha suala la afya wanaliopa kipaombele kikubwa sana, kwakujenga vituo vya kisasa kila shehia ili kuwapunguzia mzigo akinamama na watoto kufuata huduma maene ua bali.

aliwataka wananchi kukichagua chama kake, kwani hakuna mwanafunzi atakae kwenda skuli na sare mbovu, kwani serikali yake imetilia mkazo sana suala la elimu, na kuahidi kuwapatia fomu wanafunzi wote ili kusoma kwa amani.

Mgombe ubunge kupitia chama cha NRA Khalid Makame Issa, aliahidi kulipa kifuta jasho kwa walimu wa madrasa zote za Quran, zilizomo ndani ya jimbo hilo kwa shilingi elfu 50,000/= kila wiki.

Hata hivyo alivitaka vyama vyengine kutambua kuwa NRA haitumiliwi na chama chochote cha siasa, huku akiwataka vijana kutokukubali kuingia barabarani au kukubali kuvunja amani ya nchi.

Naye mgombe uwakilishi wa jimbo la Kojani kupitia chama cha NRA, alisema imekuja kuwatatulia wananchi matatizo yanayowakabili wananchi wa Kojani, kutokana na kukimbiwa kwa miaka mingi na viongozi wanaowachagua.

Hata hivyo aliwataka wananchi na wanachama wa chama hicho, kutokufanya kosa wakati wauchaguzi utakapofika kwa kuhakikisha wanachagua viongozi wa NRA ili kupatiwa maendeleo.