BENK ya NMB Tawi la Pemba imewataka wadau wake kuendelea kufurahia huduma mbali mbali zinazotolewa na Bank hiyo, kwani imekuwa na kawaida ya kurudisha faida zake kwa jamii.
Kauli hiyo imetolewa na meneja wa Benk hiyo Pemba Hamad Msafiri, wakati wa halfa fupi ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, iliyofanyika ndani ya benk hiyo mjini chake chake.
Alisema benk hiyo imeweza kusaidia jamii kwa kutoa vitu mbali mbali, ikiwemo bati, nondo, Saruji hata madawati pale jamii inapopeleka maombi yao.
Aidha aliwashukuru wateje wao na watanzania wote kwa kuendelea kuwaamini na wafanyakazi wao kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja, sambamba na kutoa mashirikiano makubwa.
“Wateja wa NMB na wafanyakazi leo tunaungana na ulimwengu mzima kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, siku hii inaadhimishwa kila mwaka wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba”alisema.
Msafiri pia aliweza kuzindua huduma tatu za kidigitali, zenye lengo la kurahisisha mawasiliano kati ya benk na wateja, ili kutoa huduma bora ndani ya wakati.
Hata hivyo alizitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na namba maalumu ya Whatsapp +255 747 333 444 kwa jili ya mteja anyetaka ufafanuzi wahudma zao, huduma ya pili ni QR Code ambayo inatowa nafasi kwa wateja wao kutoa maoni na mapendekezo ya uboreshaji wa huduma, huduma ya tatu ni kurudisha Tokeni ya LUKU kwa wateja wanaonunua umeme kupitia NMB Mkononi.
Naye msaidizi Meneja wa benk hiyo Omar Said, aliwataka wananchi kuwa na utaratibu wakukata bima mbali mbali, kwani benk hiyo tayari imeshaanza kutoa huduma za bima.
Mmoja ya wadau wa benk hiyo Massoud Ali Mohamed, aliitaka NMB kufika vijijini kutoa elimu ya ukataji wa bima pamoja na huduma mbali mbali wanazozitoa, kwani wananchi wengi wa vijijini wanakosa huduma hizo.
“Nyote itakuwa munakumbuka chimbuko la Benk hii ilkuwa ni ya wakulima, ilikuwa ikifika vijijini kushajihisa wakulima kujiunga na kutoa mikopo kwao, sasa ni wakati wetu kurudi chini hususan vijijini”alisema.
Alisema benk ina mchango mkubwa sana katika uchumi wa nchi, ili kusaidia jamii pamoja na kuwataka kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Naye mdau kutoka jeshi la Polisi Pemba Cypriana Mushi, aliitaka benk hiyo kuendelea kujitangaza kwa jamii pamoja na kuendelea kushamasisha jamii juu ya ukataji wa bima.
Alisema bima inafaida kubwa sana kwa mwananchi anayekata huduma hiyo, pale anapopatwa na tatizo la moto au majanga ya baharini, barabarani.