Friday, October 18

Wawi kupatiwa maendeleo ya kisasa.

WAGOMBEA Uwakilishi na Ubunge jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake, wamesema iwapo wananchi watawapatia ridhaa ya kuongoza jimbo hilo, watahakikisha watahakikisha wanakuwa bega kwa bega na wananchi jimbo hilo, katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa muda mrefu.

Wagombea hao waliyaeleza hayo wakati walipokuwa wakiomba kura, wakati wa uzinduzi wa kampenzi za jimbo hilo huko katika uwanja wa Ditia Wawi.

Wamesema kuwa wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbali mbali, lakini ilani wa CCM 2020/2015 imeweka wazi kila kitu hivyo wananchi wategemee mambo makubwa.

Mgombea Uwakilishi wa jimbo la Wawi Bakari Hamad Bakari, aliwataka wananchi wa wawi kuwa kitu kimoja, kwani maendeleo hayana chama, dini, rangi wala kabila, bali ni yawananchi wote.

“lazima wananchi wa wawi tuwe kitu kimoja, nitahakikisha nawaunganisha wanawawi wote tuwe kitu kimoja, ili tuweze kuijenga wawi mpya yetu ya maendeleo”alisema.

Alisema mwaka huu sio wakati wa kuchagua CUF, ACT wazalendo na vyama vyengine bali ni wakati wa kukichagua chama cha mapinduzi ili kuletewa maendeleo.

Mgombe ubunge jimbo hilo Khamis Kassim Ali, alisema ilani ya CCM 2020/2025 haikuacha kitu, hivyo wananchi wategemee medeleo makubwa katika sekta ya elimu, ajira, afya, barabara pamoja na vijana.

Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla alisema CCM ndio chama pekee kinachoongoza nchi katika kutangaza maendeleo na ndio inayotekeleza ilani yake kwa vitendo.

Alisema CCM itaendelea kuyalinda Mapinduzi matukufu ya 1964 kulinda Muungano wa serikali mbili, pamoja na kuwahakikishia wananchi kuwa ulinzi utakuwepo kabla ya uchaguzi, baada ya uchaguzi huku vijana kibakia majumbani.

Katibu wa CCM mkoa wa kusini Pemba Mohamed Khalfan, aliwataka vijana kuendelea kudumisha amani ya nchi, kwani amani ndio kila kitu kwa sasa.

Kwa upande wake hamadi Abdalla Rashid (GEREI), aliwahakikishia wagombea uwakilishi na ubunge wa jimbo la wawi kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu, kwani mikakati tayari ameshawawekea ili kufikia malengo hayo.