Friday, October 18

Mgombe uwakilishi Ole aahidi neema

MGOMBEA uwakilishi jimbo la Ole Massoud Ali Mohamed, akiwasalimia wananchi wa jimbo la Ole, kabla ya kuzungumza nao katika mkutano wakampeni wa Chama Cha Mapinduzi jimbo hilo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

MGOMBEA Uwakilishi wa jimbo la Ole kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya ya Chake Chake Massoud Ali Mohameda, amewataka wananchi wa jimbo hilo kuhakikisha wanamchagua ili aweze kuwaletea maendeleo.

Alisema iwapo watamchagua atakua ni mwakilishi wa wananchi wote, hivyo maendeleo ni ya watu wote kwani maendeleo hayachagui chama, dini, kabila wala rangi.

Aliyaeleza hayo katika mkutano wa kampeni wa jimbo la Ole, wakati alipokua akiomba kura kwa wananchi wa jimbo hilo, kuelekea uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.

Aliwataka wazee na wanaole kuhakikisha hawapotezi bahati yao hiyo ambayo wameikosa kwa muda mferu, hivyo wanapaswa kumchagua ili kuwatumikia wanaleo.

Mgombea huyo alisema ndani ya ilani ya CCM ya 2020/2015 wananchi wa jibo la ole, vimo vipaombele vingi vinawagusa katika kupatiwa maendeleo bora, kwani wananchi wanahitaji viongozi bora watakao waletea maendeleo.

“Nimekuja kwenu kuwaombea kura nawaombeni munichague niwe mwakilishi wenu, ili niweze kuwatumikia kwa kuwaletea maendeleo katika jimbo leu”alisema.

Alisema wakati umefika sasa kwa wananchi wa jimbo la ole kubadilika, miaka 25 wamedanganywa kuwa watapatiwa maendeleo, bali maendeleo yaliyopo yametokana na ilani ya CCM ya 2015/2020, kwani changamoto zilizopo za elimu, afya , barabara na ajira alihakikisha zitawaondokea.

Akizungumzia suala la ujasiriamali, aliwahakikishia kuwapatia mikopo ambayo haitokuwa na riba kwa lengo la kuondosha kilio chao cha muda mrefu.

Katika hatua nyengingine Mgombea uwakilishi huyo, alisema CCM ni chama kinachohubiri amani, ukweli kwani wananchi wanahitaji maendeleo bora.

Kwa upande wake mgombe ubunge jimbo hilo Juma Hamad Omar, aliwataka wananchi kutokufanya makosa kama walioyafanya miaka iliopita, kuhakikisha wanawachagua viongozi wa CCM katika uchguzi mkuu wa mwaka huu.