Sunday, November 24

Wawi kutekeleza ilani kwa Vitendo.

MENEJA kampenzi za CCM Mkoa wa Kusini Pemba Mohamed Aboud Mohamed, akimnadi mgombea uwakilishi wa jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake, Bakari Hamad Bakari wakati wamkutano wa jimbo la Wawi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

MGOMBEA Uwakilishi wa jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake, kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Bakari Hamad Bakari amesema iwapo wananchi wa jimbo hilo watamchagua atahakikisha wananchi wote wanakuwa kitu kimoja katika kuleta maendeleo ya jimbo hilo.

Alisema maendeleo ya jimbo la wawi yataletwa na wananchi wajimbo hilo, iwapo watakuwa pamoja na viongozi wao waliowachangu kupitia chama cha Mapinduzi, kwani ndio wanaojuwa shida za wananchi hao.

Mgombea huyo aliyaeleza hao wakati katika mkutano wa kampeni za chama hicho, huko Matungu Wadi ya kibokoni jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake.

Alisema ilani ya CCM 2020/2025 ibara ya 136 (c) imeahidi kuzalisha ajira kwa vijana zipatazo 300,000 kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi ifikapo 2025, ambapo zikigaiwa kwa majimbo ya Zanzibar jimbo la Wawi itapata ajira 6,000, zitakazowafika na kutoa hamasa kwa vijana na akinamama wa jimbo la wawi.

“Tuchaguweni ndugu zanguni ili tuwaletee maendeleo, vijana hii ndio fursa pekee kwetu ili tufikie malengo ambayo yaliopatikana”alisema.

Mgombea huyo aliongeza kuwa ibara ya 161, haikuacha nyuma kuwaunganisha wajasiriamali kuwa pamoja na kuunda vyama vya ushirika, ambavyo vitasaidia kutoa ajira kwa vijana na wanawake.

Alisema uwepo wa vikundi hivyo, wataweza kunufaika kupata mikopo na misaada mbali mbali, ambayo itaweza kuwaunua kiuchumi na kupata ajira.

Hata hivyo aliwataka wananchi wa jimbo hilo, kutokufanya kosa kibokoni vipo vikundi vya ushirika ambavyo tulivisaidiwa kipindi nikiwa mwenyekiti wa baraza la Vijana Wilaya ya Chake Chake, kwa kuwachimbia visima viwili vya maji, hivyo aliwataka kuitumia fursa hiyo adhimu kwao.

Akizungumzia suala la elimu, alisema Alisema pia ibara ya 182 imeelezea suala zima la elimu, hivyo atahakikisha tatizo la watoto kufuata nasari masafa marefu ataliondosha na watasoma kibokoni.

Akizungumzia barabara ya kibokoni, alisema iwapo watamachangua ataishawishi wizara husika kuitengeneza kwa kiwango cha lami barabara hiyo, pamoja na kutumia fedha za mfuko wajimbo.

Naye mgombe aubunge jimbo hilo, Khamis Kassim Ali, aliahidi kuwafuta machozi wananchi wa jimbo hilo la wawi, kwa kuwatekelezea kwa vitendo mambo yote yalioelezwa kwenye ilani ya CCM 2020/2025.