Friday, January 24

PBZ Tawi la Wete imeadhimisha siku ya wateja.

 

BENK ya watu wa Zanzibar PBZ Tawi la Wete, imeadhimisha siku ya wateja wa Benk, kwa kujumuika na wateja wao na kuwashukuru kwa kuendelea kuwa na imani na benk yao.

Tawi hilo lenye maskani yake bopwe Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, imeadhimisha siku hiyo kwa ukataji wa keki na kujumuika na wateja wake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kaimu meneja wa benk hiyo Ahmed Abubakar Mohd, aliwashukuru wateja wa benk hiyo kwa kuendelea kuwa na imani na benk yao, na kuahidi kuwahudumikia kwa hali na mali.

Alisema benk hiyo imekua ikitoa huduma mbali mbali kwa jamii, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na zenye uhakika, kuhakikisha uchumi unakuwa na kufikia uchumi wa buluu.

“Sisi leo tumeona tuungane na wananchi wetu katika kuadhimisha siku ya wateja wa mabenk duniani, ni moja ya siku ambayo mabenk hukutana na wateja wake na kubadilishana mawazo, kujuwa changamoto zinazowakazwa wateja wetu”alisema.

Alifahamisha kuwa katika kufikia malengo ya benk inaswa kuwa karibu na wateja wake, pamoja na kuweza kurudisha ihsani kwa wateja, kutokana na amana zao wanazoziweka.

Hata hivyo aliwataka wananchi mbali mbali wa wilaya ya wete na Micheweni, kuendelea kuitumia benk yao ya PBZ Tawi la Wete, ili kurudisha fadhila kwa uongozi wa PBZ kuwaweka tawi hilo wete.

Naye Khamis Ali miongoni mwa wateja wa benk hiyo, aliishukuru uongozi wa PBZ Wete kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, kwani wateja huvutika na ukarimu wa wafanyakazi wa taasisi inayotoa huduma.

“Tokea kuanza kazi kwake bado sisi watu wa wete hatujasikia maneno maneno yoyote juu ya watoa huduma wa benk hiyo, mapaka sasa wanendelkea vizuri chamsingi ni kujitahidi kuwa karibu na wateja wao”alisema.

Moza Yussuf Suleiman aliutaka uongozi wa benk hiyo, kufika hadi vijijini kuelimisha wananchi juu ya uwekaji wa fedha zao benk na kuacha tabia ya kuzihifadhi majumbani.