Sunday, November 24

TASAF yawakutanisha waandishi Tanga.

WAANDISHI wa Habari kutoka Unguja, Pemba na Tanga wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Tasaf na katibu Tawala Mkoa wa Tanga Judika Omar, mara baada ya kufungulia kwa kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamu ya Tatu ya Tasaf, kikao hicho kilichofanyika halmashauri ya Jiji la Tanga.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, TANGA)

 

NA ABDI SULEIMAN, TANGA.

 

 

WAANDISHI wa habari wameshauriwa kuwashajihisha walengwa wa mpango wakunusuru kaya masikini Tanzania, kutumia rasilimali zozote zinazotolewa na mfuko wa maendeleo ya jamii Tanzania (TASAF)kuweza kuboresha maisha yao.

Ushauri huo umetolwa na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Judika Omra, wakati alipokuwa akifungua kikao kazi cha kuwajengea uwelewa, waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya Tasaf, kimewashirikisha waandishi wa habari kutoka Dar Esalam, Morogoro, Unguja na Pemba na kufanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Alisema waandishi wandishi wahabari ni watu muhimu sana, katika kuelimisha jamii katika masuala mbali mbali hivyo, wanapaswa kuwa mabalozi wazuri kwa jamii ili malengo ya Tasaf yaweze kufikiwa kwa walengwa.

“Katika awamu hii ya tatu kipindi cha Pili, nguvu nyingi zitaelekezwa katika miradi itayokayoweza kuwaondoa katika umasikini”alisema.

Alisema kipindi hiki cha pili awamu ya III ya Tasaf, itaenda hadi 2023 na inatekelezwa nchi nzima, lengo ni kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa jamii katika kupunguza umasikini.

Hata hivyo alisema waandishi kioyo cha jamii, pamoja na kuwataka kuyatumia vyema mafunzo hayo ikizingatiwa ndio wanufaika wakwanza na mafunzo ya kipindi cha pili cha Tasaf.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF)Ladislaus Mwamanga alisema lengo la kikao kazi hicho ni kujenga uwelewa kwa waandishi wa habari kujuwa shuhuli za Tasaf, kwani wao ni wawakilishi wazuri wa shuhuli za Tasaf.

“Waandishi wataweza kutoa taarifa sahihi na kuondosha upotoshaji wa utoaji taarifa, zilizozagaa ambazo sio sahihi katika jamii”alisema.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka Tasaf Makao Mkuu Tanzania, Zuhura Mdungi aliwataka waandishi wa habari kuwa mabalozi wazuri katika kuelimisha jamii juu ya mikakati na mipango yanayofanywa na Tasaf kwenye kipindi cha pili cha Tasaf III.

Aliongeza kwamba Tasaf inafanya kazi kwa kuzingatia malengo ya Serikali, hivyo waandishi ni vizuri kujiridhisha pale kwa viongozi wa Tasaf, pale wanapokusanya taarifa zao kwa walengwa wa mpango huo, ili habari itakayotoka iwe sahihi na yakuaminika.

Mratib wa Tasaf Mkoa wa Tanga Ramadhan Ali, alisema Tasaf imeamua kukutana na waandishi wa habari kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania, ili waweze kuelimisha jamii kwa usahihi juu ya mikakati ya mfuko huo kipindi cha pili kwa walengwa wa kaya masikini.

“Tayari awamu hii ilishazinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mgufuli, huu ni mpango wa miaka mine kwa sasa, wanakaya lazima washiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi”alisema.

Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni mwanidhsi wa habari kutoka Gazeti la Mwananchi Lilian Lucas, alisema mafunzo hayo kwa waandishi wa habari yatawasaidia sana katika kazi zo za kila siku, kwa kuhakikisha wanaandika habari zenye tija na usahihi.

Kikao kazi cha kuwajengea uwelewa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya Tasaf, kimewashirikisha waandishi wa habari kutoka Dar Esalam, Morogoro, Unguja na Pemba.