Saturday, October 19

Wanafunzi kushirikishwa katika kongamano la Siku ya Maafa dunaini.

PICHA NO:1. WANAFUNZI kutoka skuli ya Sekondari Madungu Mjini Chake Chake, wakifuatilia kwa makini kongamano la wanafunzi katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Maafa Duniani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

 

AFISA Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Mohamed Nassor Salima amesema kushirikishwa kwa wanafunzi katika kongamano la Siku ya Maafa dunaini, litakuwa ni mwarubaini wa majanga maengine kutokea katika jamii.

Alisema hilo litatendeka, pale wanafunzi hao watakapoifikisha elimu ya maafa katika jamii iliyowazunguruka, kwa kufuata mikakati na kanuni za kukabiliana na maafa.

Mdhamini huyo aliyaeleza hayo wakati alipokuwa akifungua kongamano la wanafinzi, kuelekea siku ya maafa duniani, lililofanyika katika skuli ya Mdungu Sekondari.

“Wanafunzi hawa ni vyanzo vizuri vya kufikisha ujumbe kwa jamii, watawaelimisha wazazi wao, marafiki zao elimu itaweza kuenea kwa wingi”alisema.

Akizungumzia umuhimu wa Makongamano hiko kwa wanafunzi, alisema litaweza kuwasaidia uwezo wao wa kufikiri, namna ya kujenga hoja, pamoja na kuwasaidia katika kujibu mitihani yao ya sayansi jamii.

Aliwataka vijana kutumia nafasi hiyo kwa kuhakikisha jamii inapata elimu ya kukabiliana na maafa, kwani ndiko kwenye majanga mbali mbali, huku serikali ikihitaji wananchi wake kuishi salama.

Katika hatua nyengine Mdhamini huyo, aliwasihi wanafunzi kuacha kutumia vifaa vya umeme ndani ya madahalia yao, bila ya ridhaa ya mwalimu husika, pamoja na kuwaagiza walimu kuhakikisha mwanafunzi atakaepatikana na simu, kurudishwa kwao ili kwenda na mzazi wake.

Adha aliwataka wanafunzi kutambua kuwa kazi yao ni kusoma wanapokuwa skuli, kwani serikali imekuwa ikiwapatia huduma mbali mbali, sambamba na kuacha kuacha kujiingiza katika vishawishi vya siasa, ikizingatiwa kuwa wakati wao bado haujafika.

“Sasa hivi munatakiwa musome kwa bidii muda wa kuingia katika mambo ya siasa kwenu bado, serikali saivi imeshaongeza nafasi kwa wanafunzi watakaopata alama ya kwanza kidato cha sita”alisema.

Mkuu wa kamisheni ya kukabiliana na Maafa Pemba Khamis Arazak Khamis, alisema kamisheni ya kukabiliana na maafa imekuwa ikitoa elimu kwa makundi mbali mbali, ili kujikinga na maafa pamoja na kujuwa atathari zake.

Alisema licha ya elimu kutolewa lakini, bado baadhi ya wananchi wamekuwa wakipuuza taarifa mbali mbali zinazotolewa katika kukabiliana na maafa.

Nao wanafunzi hao waliiyomba kamisheni hiyo, kuendelea kuwalimisha wananchi kwa kuhakikisha wanafika vijijini katika kutoa elimu hiyo ya kukabiliana na maafa.

Walisema kuna baadhi ya wananchi vijijini hawajuwi hasa nini maana ya maafa, hivyo ili kupunguza au kutokomeza kabisa maafa yasitokee ni vizuri kufika huko na kuelimisha wananchi.

Katika kongamano hilo, mada mbali mbali ziliwasilishwa ikiwemo ijuwe kamisheni ya kukabiliana na maafa, Muelekeo wa mvua za Vuli Oktoba hadi Disemba 2020 na siku ya maafa duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 13 ya kila mwaka.