Saturday, October 19

Wajue ndege wenye upepo.

 

Wanyama 10 walio na kasi zaidi duniani

Baadhi ya wanyama hao huruka angani, wengine huogelea baharini na wengine hukimbia ardhini kulingana na mtandao wa OneKindPlanet unaoangazia elimu ya wanyama.

Hawa ni wanyama 10 bora walio na kasi zaidi duniani

  1. Sungura wa Hudhurungi

CHANZO CHA PICHA,DE AGOSTINI PICTURE LIBRARY

Ana miguu mirefu ya rangi nyeusi inayomuwezesha kukimbia kwa kasi ya kilomita 77 kwa saa, kasi sawa na mbwa mwitu mwekundu.

  1. Nyumbu wa Samawati

CHANZO CHA PICHA,HOBERMAN COLLECTION/GETTY

Nyumbu wa buluu, Springbok na gazelle wote wanaweza kukimbia kasi ya kilomita 80 kwa saa karibu sawa na kasi ya simba

  1. Samaki aina ya Marlin

CHANZO CHA PICHA,BBC/TWITTER

Marlin anaweza kuogelea kwa kasi ya kilomita 80 kwa saa, akinyang’anywa taji hivi karibuni na samaki aina ya Sail ambaye ndiye mwenye kasi zaidi duniani.

  1. Paa wa Pembe la Kuchoma

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Swala aina ya Pronghorn ni mnyama wa pili wa ardhini mwenye kasi ya kilomita 98 kwa saa.

  1. Samaki wa Tanga

CHANZO CHA PICHA,DOUG PERRINE/NATUREPL.COM

Samaki huyu ni mwenye kasi zaidi duniani, akiwa na kasi ndani ya maji ya kilomita 110 kwa saa.

5.Duma

 

Duma ana ujuzi katika kukimbia haraka na anaweza kufikia kasi ya kilomita 113 kwa saa.

Hiyo ni kasi kubwa mara tatu ya binadamu ambaye ana uwezi wa kukimbia kilomita takribani 36 kwa saa . Duma wana ujuzi kuliko mnyama mwingine wa aina yake.

  1. Bata bukini- mwenye mabawa ya ncha

CHANZO CHA PICHA,DEA / JACCOD/GETTY IMAGES

Bata bukini ni bata mkubwa duniani anayeweza kupaa kwa kasi ya kilomita 142 kwa saa.

  1. Ndege Msindikizaji

CHANZO CHA PICHA,SHAYNA BRODY, WAITT INSTITUTE

Hukimbia umbali wa kilomita 153 kwa saa anasaidiwa na urefu wa mabawa yake ukioanisha na uzito wa mwili wa ndege yoyote. Ndege hawa wana uwezo wa kukaa angani kwa zaidi ya wiki moja.

  1. Ndege aina ya Spine Tailed Swift

CHANZO CHA PICHA,DRAKULIREN/ISTOCK

Ni ndege mwenye rangi nyeupe shingoni na mkia uliochongoka, ni ndege mwenye zaidi anapopaa akiwa na kasi ya kilomita 171 kwa saa.

1.Kipanga

CHANZO CHA PICHA,EPA

Ndiye ndege mwenye kasi zaidi, kwa hakika ndiye mnyama aliye na kasi zaidi kwenye sayari, wakati akiwa kwenye mbizi ya uwindaji, huinuka kwa umbali mrefu, kisha huzama kwa kasi ya zaidi ya kilomita 322 kwa saa.