Wednesday, January 15

DK. Shein anena Micheweni.

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamedd Shein, akiwahutubia wanachama cha Mapinduzi Wilaya ya Micheweni wakati wamkutanpo wa kampeni wa CCM, uliofanyika uwanja wa Shamemata Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MAKAMU mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein amesema kazi kubwa iliyopo mbele inapaswa kufanywa na wanaccm, kwa kuhakikisha wakakirudisha tena madarakani chama cha Mapinduzi na dhambi ya wanahubiri ugomvi ni kuwanyima kura.

Alisema uongozi hautaki mzaha au kujaribu, kwani wanaCCM wako makini sana ndio maana wakakamilisha utekelezaji wa ilani ya CCM ya miaka mitano iliyopita, na kufanikiwa katika mambo mengi ya maendeleo hata yakipimwa kwa kutumia mizani.

Makamu huyo mwenyekiti wa ccm Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, aliyaeleza hayo katika uwanja wa Shamemata Micheweni, wakati akiwahutubia wananchi na wanaccm wa wilaya hiyo.

Akizungumzia suala la Mapinduzi matukufu ya zanzibara ya 1964, ndio yaliyoleta ukombozi wa Zanzibar, Zanzibar ilikuwa haina maendeleo yoyote ilitupwa, ilibezwa, ilizarauliwa na kunyanyaswa, Mapinduzi lazima wafahamishwe watoto kwa kutokuyachezea licha ya kuwepo watu wanayoyachezea.

“lazima tuyaenzi, tuyatunze, tuyathamini hakuna mbadala wa Mapinduzi, bila ya mapinduzi tusinge fika hapa tulipofika leo, kila mtu yuko huru katika nchi hii”alisema.

Alisema kila ilani ya CCM inazungumia Mapinduzi hata aliyokabidhiwa Dk Hussein Ali Miwnyi inazungumia Mapinduzi, na ndio atakaeweza kuyatetea na viongozi wengine, kwani hakuna mbadala wa Mapinduzi.

“kila jambo la Zanzibar limetokana na Mapinduzi, afya, kilimo, maji, micheweni ya leo sio micheweni ilivyokuwa, hayati Mzee Aboud Jumbe ndie aliyetoa micheweni mashimoni”aliongeza.

Alieleza kwamba leo micheweni inangara na imepata bahati kubwa sana, ccm lazima irudishwe tena madarakani kwani vitu vyote vilivyoko katika wilanya nyengine na micheweni kipo.

Alifahamisha kwamba Dk.Mwinyi ndio mmoja ya viongozi wanapaswa kuchaguliwa, kwani anauwezo mkubwa wa kuiyongoza zanzibar kiutendaji, kimaadili, kufikiri na kubuni mamba makubwa wananchi wa micheweni wanapaswa kuyaendeleza mapinduzi.

Alisema Dk.Mwinyi ni msomi mkubwa sana, ni mtaalamu wa matibabu ya binaadamu ikiwemo Moyo, pia ni mwalimu wa madkatari na asio mwanagenzi wa siasa za Zanzibar, siasa zote anazijuwa hivyo wananchi mchaguweni ili apate kuwaletea maendeleo makubwa ya Zanzibar.

Dk.Shein alisema lazima wanaccm wa unguja na Pemba kuachana na mambo ya kizamani, yakale havifai tena Dk.Mwinyi ni kizazi cha sasa kinachopaswa kupewa kura.

Akizungumzia faida ya miaka 56 ya Muungano, alisema zipo baadhi ya nchi zinauwonea choyo Muungano, hivyo wanaotaka muungano uwa nchi tatu wanapaswa kupuuzwa, kwani Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hautovunjika, bali utalindwa na Dk.Miwnyi na Rais Magufuli.

Hata hivyo aliwataka wazaznibari kuendelea kushikamana, kuamianiana pamoja na kuwa waumini bora wakulinda amani na utulivu iliyopo nchini.

Kwa upande wake mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk.Hussein Mwinyi, alisema iwapo wananchi wa Zanzibar watamchagua atahakikisha micheweni inabadilika na kuwa ya kisasa.

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, akiwahutubia wananchi na wanaccm wa Wilaya ya Micheweni

Alisema moja ya malengo yake ni kuipandisha hadhi hospitali ya micheweni na kuwa ya Wilaya, pamoja na kuirasimisha bandari ya shumba mjini kuwa badari rasmi itakayoweza kutoa huduma kwa vyombo mbali mbali.

Naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Abdalla Juma Mabodi, alisema ccm inaendelea kunadi sera zake kisayansi, kwani inajivunia sana utekelezaji wa ilani yake ya miaka mitano iliyopita.

Aidha aliwataka wananchi kutokushiriki katika uchaguzi wa Oktoba 27 ambao ni watu maalumu, badala yake kushiriki uchaguzi wa Oktoba 28 utakaojumuisha watanzania wote.

Kwa upande wake mgombea uwakilishi wa jimbo la Micheweni Shamat Shaame Khamis, alisema chama cha Mapinduzi kimeweza kuibadilisha Micheweni na kuwa ya kisasa, kutokana na iwepo wa huduma mbali mbali muhimu.

Alisema maendeleo yaliyopo Micheweni hata wilaya nyengine yapo, ikiwemo hospitali ya kisasa, huduma za umeme, maji, skuli za kisasa, pamoja na barabara.