Wednesday, January 15

PBZ yawashukuru wateja wake.

 

UONGOZI wa Benk ya watu wa Zanzibar Tawi la chake Chake, umewashukuru wateja wake kwa kuendelea kuitumia kwa kueka amana zao katika benka hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na kaimu meneja wa benk hiyo Said Saleh Rashid, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kuadhimisha wiki ya wateja wa benk.

Alisema wiki ya wateja wa benk huadhimishwa duniani kote, hivyo Pbz imeona kuungana na wateja wake, ili kuendeleza utoaji wa huduma bora na kuwa nao kutokana na mchango wao kwa benk hiyo.

Kaimu meneja alifahamisha Pbz imeweza kuboresha huduma mbali mbali, kwa lengo la kuwarahisishia wateja wao kuweza kunufaika na huduma hizo.

“Sisi leo tumeona ni bora kuwa pamoja na wateja wetu katika kuzimisha wiki ya wateja wa mabenk, siku hii huadhimishwa duniani kote, wateja wataweza kututathmini utendaji wetu wa kazi”alisema.

Alisema PBZ ni miongoni mwa benk kongwe iliyoanza zamani, lakini bado wananchi wanendelea kuitiumia kutokana uwaminifu uliopo kwa wateja wake, pamoja na kusaidia jamii huduma mbali mbali.

Naye kaimu meneja wa Islamik Benk Chake Chake Ali Salim Ali, alisema huo ni utaratibu wa mabenk yote kuwa na wiki maalumu ya siku ya wateja, aliwaomba wateja kuwa karibu nao kutumia huduma zao.

Alisema benk hiyo ya kiislamu inatoa huduma mbali mbali, ikiwemo mukopo isiyo na riba, mikopo ya elimu kwa wanafunzi ambao wanaenda kusoma sio mabenk mengi ambayo yanatoa huduma hiyo.

“Mikopo mbali mbali inayotolea na benk hii haina riba, hivyo ni vizuri wananchi kujitokeza kuinga mkono benk yao ya kiislamu hapa pemba”alifahamisha.

Naye Ramadhani Omar Khamis miongoni mwa wateja wa benk hizo, alisema benk hizo zinatoa huduma bora na nzuri, huku akiwataka wananchi wengine kutumia benk kuhifadhi amana zao na sio kuziweka majumbani ambako usalama ni mdogo wa fedha.

Riziki Ali Salim alisema Islamik benk ni benk nzuri inayotoa huduma bora, benk isiyonariba katika mikopo yake na kuwataka wananchi kujitokeza kuitumia benk hiyo.