CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Mlipuko wa nyota kubwa angani huenda unachangia wingi wa dhahabu, lakini haitoshi
Kila uchao kiwango cha dhahabu ambayo haijachimbwa kinaendelea kupungua duniani.
Kiwango cha dhahabu ilichosalia duniani kinakadiriwa kuwa karibu tani 50,000, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wanajiolojia wa Marekeni.
Tafiti zilizofanywa awali zilibaini kuwa dhahabu haiwezi kukuzwa upya.
Hata hivyo tafiti tofauti katika miaka ya hivi karibuni zimefichua kuwa kuna hifadhi kubwa ya dhahabu nje ya sayari ya dunia.
Inasadikiwa kuwa kiwango hicho kikubwa cha dhahabu ambacho sio ya kawaida imewafanya wanasayansi kukuna vichwa kwa miaka kadhaa wakijaribu kutafuta inapatikana wapi hasa.
Ripoti iliyotolewa wiki hii inaashiria kuwa kiwango cha dhahabu iliyopo duniani ni kubwa kuliko ni kubwa kuliko kile kilichokadiriwa katika tafiti zilizopita.
Ripoti hiyo iliyochapishwa katika jarida unajimu, inasema chanzo kikuu cha dhahabu duniani kufikia sasa ambacho- mgongani wa nyota ya neutroni – haitoshi kuelezea kiwango cha chuma kilichopo duniani na angani.
“Dhahabu na madini zingine nzito hutengenezwa kutokana na kadhaa inayohusisha nguvu nyingi katika Ulimwengu. Hatahivyo kulingana na mifano ya sasa, michakato hii haitoshi kutoa dhahabu yote tunayoiona katika Ulimwengu leo, “alisema. Mtaalam wa nyota Chiaki Kobayashi, kutoka Chuo Kikuu cha Hertfordshire na kiongozi wa utafiti huo, aliiambia BBC
Kwa Kobayashi, madhumuni ya utafiti huu ni kupata habari sahihi zaidi kuhusu asili halisi ya kile kinachoitwa “chuma nzito”.
“Sio tu kuhusu dhahabu, ambayo ni sehemu ya mambo mengi katika maisha yetu. Lakini pia kuhusu kalsiamu, kwa mfano, ambayo pia anaundwa kutokana na mlipuko wa nyota,” alisema.
Dhahabu hutengenezwa vipi ulimwenguni?
Dhahabu inahitajika sana kwa uwekezaji, pia ni ishara ya hadhi na sehemu muhimu katika bidhaa nyingi za elektroniki.
Lakini je, ilitoka wapi na ilifika vipi duniani ?
Ili kuunda chembe moja ya dhahabu ni muhimu kuunda viini vya atomiki vyenye protoni 79 na nyutroni 118 kila moja.
“Hiyo inamaanisha kuwa mchanganyiko wa nyuklia lazima ufanyike hali ambayo huenda zaidi ya uwezo wa mwanadamu. Na ingawa hutokea katika Ulimwengu, haifanyiki mara kwa mara, na zaidi ya yote, haifanyiki karibu, “anasema mwanasayansi huyo.
Maelezo ya picha,
Inakadiriwa kuwa bado kuna tani 50,000 za dhahabu zilizobaki Duniani
Migongano mingi ya nyota angani ambayo ina madini ya dhahabu iliishia kuanguka duninai wakati ilipokuwa inaundwa.
Na hiyo imekuwa hadi sasa asili inayokubalika ya uwepo wa dhahabu Ulimwenguni na kwenye sayari yetu. Walakini, kulingana na utafiti wa Kobayashi, lazima kuwe na vyanzo vingine ambavyo vinazalisha kile kinachoitwa “wingi wa dhahabu.”
Lakini je, unaweza kubaini chanzo kingine ni kipi?
“Uwezekano mwingine ni ikiwa supernova itaiangamia. Inasadikiwa kuangamia kwake kunaweza kutengeza kiwango kikubwa cha dhahabu kwa muda mfupi, japo bado haitoshi, ” anaelezea Kobayashi.
Mwanasayansi huyo anafafanua kuwa uvumbuzi uliobainiwa na kundi lake unasema kuwa mabaki ya mlipuko wa nyota angani (supernovae) inakaribia kuangamia, japo kiwango kilichosalia ni kikubwa kiasi cha kutengeza vyuma vizito, mchakato wake unafanya kazi dhidi ya uzalishaji huo angani.
” Wakati nyota kubwa zinapogongana na kuanduka husababisha shimo nyeusi ambayo huishia kufyonza kile kilichotengezwa,” anafafanua.
Kile ambayo timu ya Kobayashi ilibaini kwa uhakika ni kwamba wakati nadharia ya migongano ya nyota za neutroni ingekuwa “imeunda dhahabu nyingi” ilikuwa sahihi, bado utafiti zaidi ulihitajika kufikia matokea hayo.
Maelezo ya picha,
Mgongano wa nyota ya Neutron unasadikiwa kuwa moja ya asili kuu ya dhahabu katika Ulimwengu
“Utafiti huo unajumuisha vipimo na data kutoka kwa zaidi ya makala 340 ya kisayansi ambayo yanaelezea jinsi vitu vya kemikali vinaibuka, ndiyo sababu tuliweza kufikia hitimisho lingine muhimu, “anasema mwanasayansi huyo.
Kutokana na data hizo waliweza kuelezea muundo wa vitu kama kaboni 12 na urani, mionngoni mwa zingine.
“Kwa mfano, mfano tuliouunda uliweza kuhesabu kiwango cha madini ya strontium inayozalishwa na mgongano wa nyota ya nyutroni, ambayo inalingana na kiwango ambacho wanajimu wanacho sasa, “alisema,” .
Lakini asili ya kiwango kilichopo cha dhahabu bado haijulikani.
Je dhahabu iko?
Mfano ulioundwa na timu ya Kobayashi ulitumiwa kuhesabu kiwango kilichopo cha dhahabu , japo kwa kisia:
“Kwa mujibu wa mfano wao, kiwango kikubwa cha dhahabu kupatikana duniani ni bilioni 13.8 sawa na 4.0 × 1042 kg, ambacho ni kati ya asilimia 10 -20 ya kile kinachotarajiwa katika vimondo, jua na nyota zilizo karibu “, anaelezea mwanasayansi huyo.
Maelezo ya picha,
Ni vigumu kuzalisha dhahabu kisayansi duniani.
Lakini anafafanua kuwa hii inategemea vipimo ambavyo vinaweza kufanywa kuhusu Ulimwengu leo.
“Ulimwengu unaweza kuwa hauna mwisho(hatujui kwa hakika), lakini tuna uwezo wa kuona sehemu yake. Hiyo ndiyo sababu hesabu zetu zimetupatia nambari hizi,” anasema.
Na ikizingatiwa upungufu wa dhahabu wa siku zijazo duniani, utafiti wake huenda ukatoa nafasi ya kufanywa kwa uchunguzi wa ikiwa kuna uwezekano wa kupatikana kwa madini hiyo ya thamani ulimwenguni.
“Ni vigumu,” anatilia shaka mtaalamu huyo. “Kwasababu japo kuwa jua, kwa mfano, lina kiwango cha haja cha dhahabu, ukweli ni kwamba baadhi ya migongano wa nyota ambayo huchangia kutengenezwa kwa dhahabu angani iko mbali sana kufikiwa na binadabu.”