Saturday, October 19

Shuhuli za kijamii zarejea Pemba..

 

SHUHULI mbali mbali za kijamii ambazo zilisimama tokea Oktoba 27 mwaka huu, katika maeneo mbali mbali ya Kisiwa cha Pemba sasa zimerudi katika hali yake asili.

Shuhuli hizo ikiwemo huduma za usafiri wa barabarani, maduka ya biashara, pamoja na wafanya biashara mbali mbali wadogo wadogo nao wamejitokeza kwa wingi katika mji wa Chake Chake.

Shuhuli hizo zilisimama kwa kupisha kura ya mapema ya Oktoba 27 na upigaji wa Kura Oktoba 28 mwaka huu, ili kutoa nafasi kwa wananchi kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Mwandishi wa habari hizi alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wananchi, walisema kwa sasa hakuna haja ya kuendelea kusimama kwa shuhuli za kijamii, wakati uchaguzi umeshamalizika na washindi wameshatangazwa.

Khamis Ali Mwalimu mfanya biashara wa Embe katika soko la Matunda Chake Chake, alisema kwa sasa hali iko salama na wananchi wamelazimika kuto.

“Mimi hapa nipo toka Oktoba 30 nipo na biashara yangu ya embe, wateja jana hawakuwa wengi ila leo Jumamosi watu wengi wamejitokeza, wanahitaji embe kwa ajili ya kutumia majumbani”alisema.

Alisema tokea uchaguzi ulipoanza siku tatu hakuweza kuuza biashara yake, hali iliyoanza kumtia wasiwasi kuanz akuharibika kwa embe zake.

Omar Iliasa Asaa (jina sio lake)ambaye ni mfanya biashara wa Chakula eneo la Machomanne, alisema tokea alipofunga duka Okatoba 26 hakuweza kufungua tena hadi Oktoba 31 kwa jili ya kuhofia kuvamiwa biashara yake, kama kungetokea kwa vurugu kwenye uchaguzi.

“Hakuna hata mmoja aliyetegemea kama uchaguzi utapita salama, tunajua panapokuwa na uchaguzi kuna baadhi ya wafuasi wa vyama hawatokubali na kufanya vuru, ndio tukafunga baishara zetu kwa ajili ya usalama”alisema.

Hata hivyo alifahamisha kuwa baada ya hali kutulia, wamelazimika kufungua maduka na wananchi wamejitokeza kwa wingi kufuata mahitaji yao ya majumbani.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, aliwashukuru wananchi wa Pemba kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa salama na amani, pamoja na kuendeleza utulivu wan chi baada ya kumalizika kwa uchaguzi.

”Kwa sasa hali iko vizuri, utulivu na mkoa upo salama, wananchi wanahitaji maendeleo, niwakati wakusubiri maendeleo kwa sasa kutoka kwa Dk Mwinyi”alisema.

Aliwataka wananchi kuendelea kudumisha amani ya nchi, kwa kuhakikisha shuhuli za maendeleo zinaendelea, huku akiwataka wafanya baishara na watoa huduma za usafiri kurudisha shuhuli zao huduma kama zamani.

Msadizi Kamishna wa Polisi na kamanda wa Polisi Mkoa Ahmed Khamis Makaran, alisema tokea kuanza kwa kampenzi za uchaguzi makosa ya wizi, kujamiani na madawa ya kulevya yamepungua kutokana na kuwepo kwa hali ya ulinzi katika maeneo mbali mbali ya mkoa huo.

Alisema makosa ya kisiasa ya kuchana picha za wagombea, kutoa lugha chafu pia yamepungua, ukiachia oktoba 26 hadi 29 shida ni wafuasi wa vyama kujikusanya kwa wingi, katika vituo vya kupigia kura hadi kuwatia hofu maafisa wa uchaguzi.

Hata hivyo alisema watu kadhaa wanashikiliwa katika vituo vya mkoani na chake chake, ambao walisababisha vurugu katika vituo vya kupigia kura, huku akiwataka wananchi wa Mkoa wa kusini Pemba, kufungua ofisi zao kwani hali iko shuari kwa sasa.