Saturday, October 19

ZECO kufikisha umeme vijiji vipya Makoongwe.

 

SHIRIKA la Umeme Zanzibar ZECO Tawi la Pemba, limewataka wananchi wa Kisiwa cha Makoongwe Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kuisni Pemba, ambao hawajapatiwa huduma ya umeme kuanza maandalizi ya kupokea huduma hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mipango na utafiti shirika la umeme Tawi la Pemba Ali Faki Ali, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Makoongwe, kufuatia kukubalia ombi lao la kupatiwa umeme kwa njia ya mkopo kama ilivyokuwa kwa wenza wao mwaka 201/2015 ulipofikisha umeme kisiwani humo.

Alifahamisha mwaka huo vijiji vyote vilivyomo ndani ya kisiwa hicho walipatia huduma hiyo, lakini sasa tayari kumeshakuwa na vijiji vipya vinavyohitaji huduma hiyo, huku watu 126 wapo tayari kwa hatua ya kwanza kupatiwa umeme huo.

“Shirika limekubali ombo lenu mulilolitoa septemba 29 mwaka huu, kuwa kuna kijiji kipya cha Kinazini kinahitaji huduma hiyo, mwaka ule tunaleta umeme hakikuwemo sasa ombi lenu limekubalia, anzeni kujiandaa kupokea huduma hiyo”alisema.

Alisema wananchi hao watapatiwa huduma ya umeme kwa njia ya punguzo, kulipata shilingi laki moja (100,000) kitakachobakia watalipa kidogo kidogo mpaka watamaliza deni lao.

Aidha aliwataka wananchi kufahamu kuwa, lengo la shirika ni kutoa huduma kwa wananchi wote, kuhakikisha wananufaika na huduma ya umeme, hivyo wananchi wananpaswa kulinda na kuitunza miundoimbinu ya umeme.

Kwa upande wake afisa uhusiano na huduma kwa wateja wa ZECO Pemba Amour Salum Massoud, alisema mashirikiano yaliyopo baina ya wananchi wakiwemo kutoka kisiwa cha makoongwe, ndio yatakayosaidia shirika hilo kupiga hatua kimaendeleo.

Aliwasihi wananchi kuilinda miundombinu iliyopo ya umeme, ili kuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na kizazi kianchokuja, kwa kunufaika na huduma ya umeme wa uhakika.

Alifahamisha kwamba wapo baadhi ya wananchi wanachimba mchnga karibu na nguzo za umeme, pamoja na wale wanaochukua mchanga baharini ambapo kebo ya umeme mkuba imepita.

“kuna watu wanatafuta hatari tena kuba, kuchukua au kuchimba mchanga katika maeneo ambayo kebo imepita ni kutafuta hatari kubwa, unaweza kufa ww na sisi ukatutia hasara kutafuta b=kebo nyengine, tuweni majini sana kufanya kazi zetu katika eneo ilipopita laini kubwa ya kebo”alisema.

Alisema changamoto nyengine ni ukataji wamiti katika laini kubwa za umeme, jambo ambalo linaweza kuhatarisha maisha ya wananchi husika na kusababisha majanga baadae.

Nao wananchi wa kijiji cha kinazini wamelishukuru shirika la umeme, kwa kuwafiukiria na kuwakubalia kilio chao cha kuwapatia huduma ya hiyo ya umeme kwa njia ya punguzo.’

Khalfan Kombo Mussa aliwaomba watendajani wa ZECO kupita katika kijiji hicho kuhakiki nguzo, ambazo zimeshaanza kuharibika kwa kuhofia kuanga kwenye majumba ya wananchi.