Saturday, October 19

Walimu Mkoani waipongeza UNESCO.

 

WALIMU wa skuli za msingi na Sekondari Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba, wamelipongeza shirika la Umoja wa Mataifa elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO)Tanzania, kuingiza wilaya ya mkoani katika wilaya nne za Tanzania katika mradi wa majaribio wa Stadi za Maisha, Ukimwi, afya ya Uzazi na Elimu ya Jinsia.

Walimu hao wamesema kuwa hatua hiyo ya wilaya ya mkoani imekuwa na habati ya pakee, kunufaika na mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika ufundishaji wa wanafunzi maskuli.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, huko katika skuli ya Mohamed Juma Pindua Chokocho Wilaya ya Mkoani, mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku sita ya kuwajengea uwezo walimu 15 za wilaya hiyo.

Mwalimu wa ushauri skuli ya Sekondari Mkanyageni Time Mohamed Shamuuni, alisema changamoto kubwa ni tabia mbaya ambazo zimeibuka tafauti tafauti zilizoanza kuleta athari ambazo zinahitaji kurekebishwa.

 

Alisema katika kufanikisha hilo atahakikisha anashirikiana na walimu wenzake, ili kuhakikisha wanafunzi wanaondokana na vishawishi, kwani vishawishi hupelekea kufanya vibaya katika masomo yao.

“Mafunzo ya mara kwa mara ndio yanayoimarisha utendaji wa kazi za kila siku, wafanafunzi nao wataweza kuhamasishwa kuachana na matuko maovu”alisema.

Aidha akizungumzia suala la usafi kwa watoto wakike, alisema changamoto kubwa ni haba wa maji katika skuli nyingi, kwani bila ya maji usafi vyooni itakuwa ni tatizo.

Muhsini Salim Faki alisema mwalimu ni mlinzi wa wanafunzi maskulini, hivyo elimu hiyo inawasaidia kujua matatizo yanayowasibu wanafunzi, ikizingatiwa baadhi ya wanafunzi huwa wasiri kueleza matatizo yao.

Aidha mwalimu Muhsini aliishukuru UNESCO na KOICA kwa kuratib programa hiyo, ambayo ya kuwafunda walimu juu ya masuala ya Stadi za Maisha, Ukimwi, afya ya Uzazi na Elimu ya Jinsia.

Hata hivyo aliwataka wanafunzi kutambua wajibu na nafasi yao katika suala zima la kutafuta elimu, huku wakiachana na mambo ambayo hayanania njema na wao.

Kwa upande wake afisa elimu sekondari Mkoa wa kusini Pemba Mwalimu Haji, alisema mafunzo hayo kwa walimu yatawasaidia wanafunzi kuondokana na masuala ya unyanyasaji, baada ya walimu hao kuifikisha elimu hiyo kwa jamii iliyoizunguka.

Alisema atahakikisha Wizara ya welimu inawafuatilia walimu hao, kwa kuhakikisha elimu hiyo inafikishwa maskulini kwa wanafunzi ili lengo lililokusudiwa linafanikiwa.

mratibu wa miradi kutoka shirika la UNESCO Tanzania, Viola Muhangi alisema mafunzo hayo ya ni muhimu kwa walimu, katika kuwasaidia wanafunzi wao kuweza kufikia malengo yao ya kielimu, kwani wananfunzi wengi wamekuwa wakikatisha ndoto zao mapema.

Alifahamisha kuwa wilaya ya mkoni ndio wilaya ya kwanza kwa Zanzibar kunufaika na mafunzo hayo, kwenye wilaya nne za Tanzania hivyo walimu wanakila sababu ya kujifunza mbinu mbali za kuwasaida wanafunzi.