Wednesday, January 15

Wizara yakabidhi vifaa vya ushoni kwa vijana.

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othaman, akimkabidhi vifaa vya ushoni vya wilaya ya Wete Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Salam Mbarouk Khatib, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Wete, vifaa vilivyotolewa na wazara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, huku Afisa Mdhamini wa Wizara hiyo Fatma Hamad Rajab akishuhudia zoezi hilo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WIZARA ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, imekabidhi vifaa mbali mbali vya ushoni kwa viongozi wa Wilaya nne za Pemba, kwa ajili ya vijana waliomaliza mafunzo ya ushoni Kisiwani hapa, kwa lengo la kuendelea ujuzi wao huo pamoja na kujikwamua na umasikini.

Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa ni pamoja na vyarahani 76 Butterfly na Sinja, overlock 12, Pasi 20, Mikasi 123, trpu 72 na Juki 12 ili kuwasaidia vijana hao kufikia malengo yao ikiwemo kushona bila ya usumbufu.

Akitoa maelezo juu ya utoaji wa msaada huo kwa vijana, afisa Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba Fatma Hamad Rajab, alisema utoaji wa mssada huo kwa vijana umetokana na mipango madhubuti ya Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Shein, katika kuwasaidia vijana wa Zanzibar kupitia program ya vijana.

Alisema katika utekelezaji waprogram hiyo mwaka jana waliweza kutoa vifaa mbali mbali vya kilimo kwa vijana na awamu ya pili wametoa vifaa vya ushoni, ambapo bilioni 3 zimetengwa katika utekelezaji wa program hiyo.

Alifahamisha wizara iliweza kuwapatia vijana mbali mbali mafunzo ya ujasiriamali juu ya ushoni, katika chuo cha amali Vitongoji ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana.

“Vijana kile kilio chenu cha muda mrefu cha kutokua na ajira sasa kitakuwa kimeondoka, vifaa hivi kama mutavitumia kwa lengo zuri basini ajira pekee”alisema.

Alifhamisha kuwa kwa awamu ya kwanza vijana wameweza kujifunza kushona, huku kukiwa na mikakati ya kutoa elimu nyengine kwa vijana wengine.

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano ya Vifa, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othaman, aliwapongeza vijana waliokubali kujifundisha ushoni, huku akiwataka kuvitumia vifaa hivyo kwa umakini na kuwaletea tija kwao.

Alisema lengo la serikali unapopatiwa vifaa kwenda kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa na sio kuvifungia majumbani jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za serikali.

“Wasimamizi hakikisheni munavifuatilia kwa ukaribu vifaa hivi, ili tuone maendeleo yake kwa vijana hawa wanaokabidhiwa, hii ni ajira tosha na sio zalima usubiri kazi kutoka serikalini”alisema.

Hata hivyo aliwataka vijana kurudisha fadhila kwa serikali kwa kuhakikisha wanafungua sehemu maalumu kwa ajili ya kuweka viwanda vya kushonea nguo, kutokana na ujuzi wao waliojifunza vyuoni.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wakuu wa wilaya nne za Pemba, mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadidi Rashi, aliwataka vijana hao kuvitumia vifaa hivyo kwa lengo lililo kusudiwa.

Alisema viongozi wa wilaya watahakikisha wanavifuatilia kwa umakini mkubwa sana, juu ya maendeleo ya vifaa hivyo ambavyo wamepatia.

Kwa upande wao vijana wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwapatia vifaa hivyo vya ushoni, vifaa mbavyo vitawasaidia katika kujikwamua na umasikini.