Wednesday, January 15

Kiwango cha madini ya uranium cha Iran kimepita mara 12 ya kiwango kinachohitajika, yasema IAEA

CHANZO CHA PICHA,EPA Maelezo ya picha, Since last year, Iran has been reneging on its commitments under a 2015 nuclear deal Iran sasa ina zaidi ya mara 12 ya kiwango cha urutubishaji wa uranium chini ya mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 na mataifa yenye nguvu, limesema shirika hilo la dunia la udhibiti wa nyuklia

Shirika la Kimataifa la nishati ya atomiki (IAEA) limesema kuwa akiba ya uranium ya kiwango cha chini imefikia kilo 2,442.9 mwezi huu.

Iran inasisitiza kuwa mipango yake ya nyuklia ni ya malengo ya amani tu. IAEA pia ilisema kuwa maelezo ya Iran kwa ajili ya uwepo wa nyuklia katika eneo ambalo haijalitangaza wazi ”sio ya kuaminika”

Kwenye ujumbe wa Twitter, balozi wa Iran katika IAEA, Gharib Abadi, alisema kuwa “kauli zozote za haraka zinapaswa kuepukwa”, akiongeza kuwa: “mazungumzo yanaendelea kwa lengo la kukamilisha azimio la suala hilo .”

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Iran’s low-enriched uranium stockpile was limited to 300kg for 15 years under international agreement

Katika ripoti yake ya hivi karibuni, iliyosambazwa kwa wanachama, IAEA kutambua eneo ambako ilipata vifaa vya nyuklia.

Chanzo ambacho hakikutajwa kililiambia shirika la habari la AFP kwamba hapakuwa na kiashiria chochote kwamba havikutumiwa katika urutubishaji wa uranium, lakini vinaweza kuwa vilitumiwa kutunza nyuklia.

IAEA liliongeza kuwa Iran inaendelea kurutubisha uranium kutakatisha hadi kwa kiwango cha 4.5% – katika ukiukaji wa 3.67% ya mapatano chini ya mkataba wa mwaka 2015.

Shirika hilo bado linachunguza sampuli zilizochukuliwa mwezi Septemba kutoka katika maeneo ya awali yaliyoshukiwa kuwa ni ya nyuklia, ambayo yalifunguliwa kwa ajili ya wakaguzi mwaka huu.

Mwaka jana, Iran ilianza makusudi na hadharani kukiuka ahadi zake chini ya mkataba wa kimataifa wa nyuklia iliousaini na China, Ufaransa ,Ujerumani, Urusi, Uingereza na Marekani .

Hatua hiyo ilichukuliwa katika kujibu baada ya rais wa Marekani Donald Trump kujiondoa katika mkataba wa nyuklia na kurejesha vikwazo vya kiuchumi dhidi yake.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Chini ya makubaliano hayo, Iran inaruhusiwa tu kuzalisha kilo 300 za uranium katika eneo maalumu ambalo ni sawa na kilo 202.8 za uranium.

Urutubishaji wa kiwango cha chini cha uranium – ambao ni kiasi cha kati ya 3% and 5% na kiwango cha kemikali ya isopotu U-235 – ambayo inaweza kutumiwa kuzalisha mafuta kwa ajili ya viwanda vya nishati. Kiwango cha uranium inayotengeneza silaha huwa ni kinarutubishwa kwa 90% au zaidi.

Muda mfupi baada ya kutolewa kwa ripoti ya IAEA , Mfalme Salman wa Saudi Arabia – hasimu wa Iran katika kanda hiyo – alisema katika hotuba yake kwamba dunia inapaswa kuidhinisha “msimamo wa maamuzi ” ili kuhakikisha Tehran haipati silaha za maangamizi.

“Ufalme unasisitiza hatari za mradi wa Iran kwa kanda , uingiliaji wake katika nchi nyingine, unachochea ugaidi, inawasha mioto ya kidhehebu na miito ya msimamo kutoka kwa jamii ya kimataifa dhidi ya Iran inadhihirisha jinsi inavyoshugulikia juhudi zake za kupata silaha za maangamizi na kutengeneza mpango wake wa makombora yake,” alisema.

Wakati wa mkutano na mkuu wa Umoja wa mataifa, balozi wa Iran Majid Takht Ravandchi alisema nchi yake na IAEA “wamekubaliana kufanya kazi pamoja kwa uaminifu mzuri” na kutatua maswali yanayojitokeza.

Rais mteule wa Marekani Joe Biden ameashiria utashi wa Marekani wa kujiunga na mkataba wa nyuklia, na kuipa Iran “njia nzuri ya kurejea katika diplomasia .”

Jumatano, rais wa Iran Hassan Rouhani alisema kuwa nchi yake itatumia “fursa yoyote ” ku “ondoa shinikizo la vikwazo kutoka mabegani mwa watu wetu “.