Saturday, October 19

JET yampongeza Rais Magufuli.

 

CHAMA Cha Waandishi wa Mazingira Tanzania (JET) kimempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, kwa kuchaguliwa tena kuiyongoza Tanzania katika kipindi chake cha pili cha miaka mitano.

Kwamujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho Tanzania John Chikomo, Jijini Dar Esalaam kwa vyombo vya habari, imesema kuchaguliwa kwa Rais Magufuli kuiyongoza tena Tanzania ni ishar ya matumaini mema, na imani ya hali ya juu waliyonayo wananchi wa Tanzania kwake.

Mkurugenzi huyo alisema Dk Magufuli akilihutubia Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliweza kuelezea vipaombele mbali mbali, ambavyo vinagusa moja kwa moja masuala ya Mazingira, kama juhudi za kuendeleza matumizi ya nishati Jadidifu nchini pamoja na sekta ya Utalii.

Chikomo alisema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita JET, imekuwa ikiwaelimisha wananchi kuhusu faida za matumizi ya Nishati Jadidifu, kulinda wanyamapori na kukuza utalii nchini.

“Mwaka uliopita tulikuwa na mafunzo kwa waandishi wa habari, juu ya masuala ya Nishati Jadidifu kwa kushirikiana na Nukta Africa, tuliweza kufanya kazi kubwa katika sekta hiyo, ndio maana Rais Dk.Magufuli pia amezungumzia hilo na kutupa matumaini”alisema.

”Sisi JET tunampongeza Dk.Magufuli kwa hutuba yake nzuri iliyojaa matumaini kwetu katika suala zima la kulinda mazingira”alisema.

Aidha alisema JET inaendelea kuwa na matumaini makubwa na uongozi wake, katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii, sambamba na kulinda, kuhifadhi, Mazingira, utawala bora, utawala wa sheria na uwajibikaji.

JET inatambua kuwa dhamana aliyopewa Rais Dk.Magufuli na Watanzania ni kubwa, ili kuitekeleza kikamilifu dhamana hiyo inahitaji kumtanguliza mbele Mwenyezi Mungu, pamoja na kuonyesha mashirikiano kwa watanzania wote.

“JET inamwomba Mwenyezi Mungu amjalie afya njema, hekima na maarifa zaidi ya kuweza kulitumikia Taifa letu, pamoja na nguvu”alisema.

Hata hivyo alisema JET inaamini kwamba baada ya Rais kulihutubia Bunge la 12 hivi karibuni, kilichobaki sasa ni kuzidisha mshikamano na ushirikiano, katika kuijenga nchi ta Tanzania.

Chama cha Waandishi wa Habari za mazingira Tanzania, kimewataka watanzania na wadau wote wa maendeleo kutoa ushirikiano na kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.

Hata hivyo JET kinawatakia kila la kheri Rais Dk.Magufuli na  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, katika kutekeleza majukumu yao katika kipindi cha miaka mitano 2020–2025.