Kijana Khamis Shaib Khatib mwenye umri wa miaka 24 mkaazi wa Kizimbani Wete Pemba ahukumiwa kwenda chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka saba [7] na kutozwa faini ya shilingi laki mbili za kitanzania baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka msichana wa miaka kumi na tatu [13].
Hukumu hiyo imesomwa na hakimu Abdala Yahya Shamuhun baada ya kuona ushahidi uliotolewa mahakamani hapo unaridhisha.
Hakimu huyo alimtaka mshitakiwa huyo kwenda kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka saba [7] na kutozwa fidia ya shilingi laki mbili baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa la kubaka.
“Mtuhumiwa umepatikana na hatia kwa kosa la kubaka utatumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka saba[7]” alisema shamuhun.
Kabla ya kusomewa shitaka lake hilo mshitakiwa alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliomba mahakama impunguzie adhabu, ombi hilo lilipingwa na upande wa mashtaka.
“Muheshimiwa hakimu naomba munipunguzie adhabu kwani sitorudia tena kosa hili” alieleza mshitakiwa huyo.
Mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka [dpp] ali amour makame aliomba mahakama kumpa adhabu kali mshitakiwa huyo ambapo hilo litakua ni funzo kwa wengine.
Ilidaiwa mahakamani hapo siku isiofahamika mwezi 11/2019 majira ya sa 3; kamili za asubuh huko Kizimbani Wilaya ya Wete Pemba ulimbaka msichana wa miaka 13, kufanya kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 108 [1], [2], [e] na 109 [1] sheria nambari 6/2018, sheria ya Zanzibar.