Sunday, October 20

Makamo wa pili atoa agizo kwa wizara ya afya Pemba.

 

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, amemuagiza Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya dawa Zanzibar kuharakisha utaratibu wa upatikanaji wa dawa katika bohari kuu ya dawa Pemba.

Alisema bohari ya dawa Pemba imegharimu fedha nyingi na kufunguliwa karibuni, itakua haina maana ya kasi yote iliyofanywa na serikali ikaendelea kubeba gharama za lazima kuchukuliwa dawa Unguja na kuletwa pemba.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar alitoa agizo hilo baada ya kutembelea maeneo mbali mbali ya hospitali ya Wilaya ya Micheweni, pamoja na kupokea changamoto za wafanyakazi wa hospitali hiyo katika ziara yake ya siku tatu kisiwani hapa.

“Afisa Mdhamini kwa kushirikiana na mkurugenzi Tiba, hakikisheni dawa zote zinapatikana katika bohari ya dawa Pemba, sio tena kuagiza kutoka Unguja halafu tusambaze kwenye vituo, wananchi wanahitaji huduma bora na muhimu”alisema.

Alisema kama kutakuwa na masuala ya kimtandaa nao kitaalamu, vizuri yakafanyika haraka, ili dawa zieweze kupatikana katika bohari ya vitongoji na hospitali ya micheweni na nyengine za pemba waweze kufaidika na bohari hiyo.

Akizungumzia jambo jengine Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, aliuataka uongozi a Wizara ya Afya kuhakikisha wanaangalia utaratibu wa upatikanaji wa wataalamu muhimu wa kutosha katika hospitali ya micheweni.

“Kwa mfano mtu anapigwa X-Ray Micheweni, picha inaenda kusomwa na mtu mwengine katika Hospitali ya Wete au Abdalla Mzee Mkoani, huu ni usumbufu wananchi wanabebeshwa gharama ambazo sio saizi yao”alisema.

“Mkurugenzi ametwambia hapa wataalamu zaidi ya sita, wapo Unguja katika Hospitali mmoja, kuangaliwa utaratibu wa kuletwa mtaalamu mmoja wa kufanya kazi hapa micheweni”alisisitiza makamu..

Aidha aliutaka uongozi kuhakikisha wanaangalia uwezekano wakuajiri wataalamu ambao tayari wameshamaliza masomo, wapo mitaani wanazurura hatuwezi kuwaacha watu watembee na utaalamu wao, serikali hii itaendelea kusimamia juhudi za serikali kama iliyopita, kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wananchi.

Kwa upande wa Changamoto za wafanyakazi, Makamu wa Pili wa Rais Hemed, alisema stahiki za wafanyakazi, imeozoeleka kwa sasa kila kinachotokea kinaelekezwa katika Corona, Corona imekuwa kama ni sehemu ya kufichia maovu ya watendaji katika kutoa stahiki za wafanyakazi.

“Corona ilianza mwezi Machi 2020 karantini ilianza Machi 17, imeonekana hapa ni sehemu za kujifichia watu wote, madeni hayo ya wafanyakazi zaidi ya mwaka mmoja, kuna madeni makubwa sana umeme wakati fedha zilitolewa kabla ya Corona na hazijalipwa”alisema.

Alisema Hospitali imekuwa na mademi makubwa ya Umeme zaidi ya Milioni 50, Abdalla Mzee anadai Wizara ya afya Milioni 100 za umeme, hivyo ni jukumu la Wizara kuangalia bajeti zao tena zilikuwa zikipelekwa vizuri haiwezekani hospitali zikawa zinadaiwa fedha hizo.

Hata Mkurugenzi Kinga, Afisa mdhamini na Katibu mkuu wa Wizara afya, kuhakikisha wanasimamia madeni hayo na yanalipwa kwa wakati, isifike siku ikashindwa kufanyakazi hospitali kisa madeni, wakati bajeti zao madeni hayo yanakuwemo zinapoletolewa  OC fedha hizo hazipatikani, lazima fedha hizo kufatiliwa zilikuwa zinakwama wapi.

Kwa upande wa fedha za muda wa ziada kwa wafanyakazi (Coal), alimtaka Mkurugenzi Tiba na Afisa Mdhamini Wizara ya afya kuhakikisha wanatafuta utaratibu owote wafanyakazi hao ambao mwaka mmoja na nusu sasa hawajalipwa fedha zao wanalipwa.

“Ikiwa sisi haki zetu tunazipata basi na wao haki zao wanapaswa kuzipata, hatuwezi kuwafanyisha kazi kwa hali hii, halafu tuanze kuwalaumu, wewe mkurugenzi umekuja pemba umelipwa fedha zao, afisa mdhanimi unasafiri unalipwa zao, kama kujikopesha basi tuanze sisi na sio wafanyakazi”alisema.

Aidha alifahamisha kama hali ni hiyo basi bora zizuiliwe safari zote za kusafiri safari, ili wafanyakazi waweze kulipwa fedha zao wanazozidai.

Akizungumzia nyumba za maafa Tumbe, Makamu wa Pili alisema mradi huo unaendelea vizuri, huku akimtaka mkandarasi kuhakikisha nyumba hizo zinamalizwa kwa wakati muwafaka kama mkataba unavyoelekeza, ili wananchi waweze kufaidika na nyumba hizo.

Aliwataka wananchi wa Tumbe kuendelea kuwa watulivu, kwani Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amekusudia kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini.

Mkurugenzi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Makame Khatib Makame, alisema ujenzi wa nyumba hizo umefikiwa hatua za mwisho, kwani kijiji hicho kinanyuma 15 kwa familia 30 kila nyumba inaishi familia mbili, pamoja na maduka 15, skuli, kituo cha afya na msikiti.

Mkurgenzi Tiba Juma Mbwana alisema uletaji wa dawa katika kisiwa cha Pemba, zaidi huangalia zile dawa muhimu ambazo zinazohitaji ndani ya kipindi hihicho.

Kwa upande wake Daktari Dhamana Hospitali ya Micheweni Mbwana Shoka Salim, alisema katika hospitali hiyo dawa zote muhimu zinapatikana kulingana na maradhi yanayokuwepo.

Akizungumzia suala la kuwepo kwa wataalamu katika hospitali hiyo, alimuomba Makamu huyo kuhakikisha wanawapatia mtaalamu kutoka ndani ya wilaya ya micheweni, kwani kutoka maeneo mengine hawabakii na hukaa kwa muda mfupi na kuomba uhamisho huku tatizo likiwa linaendelea.

Kwa upande wa wodi ya wazazi alisema tokea kufanyiwa mabadiliko kwa sasa wanawahudumia wazazi 230 kutoka 80 hapo awali, kuhusu stahiki za wafanyakazi alisema kwa sasa hakuna stahiki zinazopatikana, tangu ki[pindi cha Corona walipopata milioni 6.

Mtaalamu wa chumba cha X-RAY Dk Ali Khamis, alisema licha ya ufanyaji kazi wa mashine hiyo, lakini bado miundombinu yake ni ya kizamani wakati sasa ni wakati wamabadiliko ya teknolojia.