Sunday, October 20

MBUNGE wa jimbo la Gando amekabidhi vifaa vya maji vyenye thamani ya Tsh 6,800,000/.

 

NA SAID ABRAHMAN.

 

MBUNGE wa jimbo la Gando kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Salim Mussa Omar, amekabidhi vifaa vya maji kwa ajili ya Kijiji cha Chozi Wilaya ya wete vyenye thamani ya Tsh 6,800,000/.

Mradi huo utahudumia wananchi wapatao 1500 wa Kijiji hicho, ambapo kwa muda mrefu wamekuwa wakihangaika na tatizo la upatikanaji wa maji.

Akikabidhi vifaa hivyo Mbunge huyo, aliwataka wananchi hao kuulinda mpira huo, ili usiweze kuharibiwa na wale wasiopenda maendeleo, huku akiwahakikishia  wananchi hao kuwa ataendelea kuwasaidia kwa kila hali itakapokuwa vizuri .

“Sisi viongozi wenu wa majimbo kazi yetu ni kuunga mkono juhudi za serikali, kwa kuwafikishia maendeleo leo tumetoa mpira huu, kazi iliyobaki ni yenu ya kulinda miundombinu hiyooo”alisema.

Aidha alisema kuwa chama cha Mapinduzi ndio chama pekee kinachojali shida za wananchi, hata viongozi wetu wa taifa wako makini katika kuwahudumia wananchi.

Nae Diwani wa wadi ya Gando Riziki Mohammed Fadhil, aliwataka wananchi hao kuwa na mashirikiano na viongozi wa jimbo lao katika kutekeleza majukumu yao.

Aidha Diwani Riziki alimpongeza Mbunge huo kutokana na kutekeleza ahadi zake ambazo alizozitoa wakati wa kipindi cha kampeni.

Nae mwenyekiti wa Kijiji cha Chozi Subira Hamad Omar, alimshukuru Mbunge huyo kutokana na juhudi zake za kuwafikishia maji katika Kijiji chao na kumuahidi kuwa wataweza kutoa mashirikiano nae katika kipindi Chake cha uongozi.