MBUNGE wa Jimbo la Chake Chake Ramadhan Suleiman Ramadhan, amekabidhi vifaa mbali mbali vya michezo pamoja na fedha taslim kwa timu zote zilizmo ndani ya jimbo hilo, kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya waligi wa 2020/2021.
Timu ambazo zimekabidhia vifaa hivyo vya michezo ni zinazoshiriki ligi daraja la kwanza kanda ya Pemba, zimepatiwa seti moja ya jezi full na mipira mitano pamoja na shilingi Laki 3.5 kwa ajili ya malipo ya ada ya msimu, huku timu za daraja la pili kanda ya Pemba zimepatiwa jezi mipira na shilingi laki 2.5 kwa ada ya msimu.
Kwa upande wa timu za darala la pili wilaya hiyo kila timu imekabidhiwa shilingi laki mmoja, huku akiwataka viongozi waliokabidhiwa fedha hizo kuhakikisha wanazifikisha katika timu zao, ili kuondosha figisu figisu zililopo.
Mbunge huyo alisema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kurudisha hadhi ya soka kwa wilaya ya chake chake, ambalo kwa muda mrefu soka lake limepotea.
Alisema vilabu haviendi mbela kwa kutokuwa na vitendea kazi, ndio wakaaza kazi kwa kutekeleza changamoto katika michezo, kwani ndiko kuliko kusanya vijana wengi ambao ndio wapiga kura.
Aidha alisema jimbo linachangamoto nyingi sio michezo tu, huku akiahidi kulipia fedha zote za usajili kwa timu zilizomo ndani ya jimbo hilo.
Hata hivo alikemea suala la ubabaishaji katika vilabu, jambo ambalo linarudisha nyuma nguvu za viongozi wanaowasaidia, huku akivitaka vilabu kujiandaa kwa mashindano ya mbunge Cup.
Naye aliyekuwa afisa mdhamini Wizara ya Vijana Pemba Fatma Hamad Rajab, aliwataka viongozi wa vilabu kutoa mashirikiano kwa viongozi wao, ili kuondosha kero zamichezo katika jimbo hilo.
Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wenzake Mzee Ali Abdalla, alimshukuru mbunge huyo, kwa kuwapatia vifaa hivyo vya michezo huku akiahidi kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa.