WAZIRI wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Mwita, amewataka vijana kisiwani Pemba kuvifanyia kazi vyarahami walivyokabidhiwa, kwa kutafuta tenda za ushonaji wa nguo ili viweze kuwasaidia katika masiha yao.
Alisema vyarahani havipaswi kukaa tu baada ya kufungwa, badala yake wanapaswa kuvitumia katika ushonaji wa vitu mbali mbali ili fedha itakayopatikana iweze kutengenezea hata ofisi yo.
Aliwayeleza hayo wakati alipokua akizungumza na vijana wa ushoni wa wilaya ya wete, huko katika ofisi za ushoni benjamini mkapa ya zamani wete.
Aidha waziri huyo alitoa wiki mbili kwa ugozi wa kikundi hicho kuanza kazi ya ushonaji, huku akiwataka kutafuta tenda kwenye maskuli kwa sasa kwa ajili ya ushoni wanguo za wanafunzi na mambo mengine.
“Serikali ya Mapinduzi imeweza kufanya kazi kubwa kwa kuwasaidia vijana, kupitia katika program ya ajira kwa jina ya bilioni tatu”alisema.
Akizungumzia kikundi cha Riziki Haina Mja cha Mjini Ole, Waziri Tabia aliwataka wanakikundi hicho kuzidisha juhudi na kuhakikisha kikundi chao kinakuwa cha mfano kwa Pemba, pamoja na kuwa chuo cha kilimo kwa vijana.
Aliwataka wanakikundi hao kuhakikisha waongeza mazao ambayo yanaendela na wakati, ili kuhakikisha wananchi wananufaika na bidhaa zao.
Kwa upande wake mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba nafasi za wanawake Asya Sharifu, aliahidi kuwasaidha wanakikundi hicho kwa kuwapatia viti vya kukalia pamoja na majora 10 ya vitambaa kwa kuanzia.
Kwa upande wake aliyekuwa afisa mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, Fatma Hamad Rajab aliwatak vijana hao kuhakikisha wanathamini mali ya serikali, ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Alisema vyarahani hivyo vimetolwa kupitia program ya ajira kwa vijana, wilaya ya wete wamekubaliana kuviweka sehemu moja ili kuwa rahisi kwao kutumia kwa kushona kwa pamojana.
Nao vijana alimuahidi Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, kuhakikisha vyarahani hivyo vitatumiwa kwa lengo lililokusudiwa, pamoja na kuwa mkombozi mkubwa kwao katika kukabiliana na ugumu wa maisha.