MKURUGENZI wa Elimu ya Msingi na Maandalizi kutoka Baraza la Mji Chake Chake Makame Pandu Khamis, amewataka wazazi au walezi kuhakikisha wanaitekeleza kwa vitendo mikaba wanayopewa skuli, wakati wanapokwenda kuwaandikisha watoto wao ili kuepuka migogoro inayotokea baadae.
Alisema kumekua na tabia ya wazazi kutokuifuata kimilifu mikataba hiyo, baada ya watoto wao kukubaliwa katika skuli walizowapeleka.
Mkurugenzi huyo aliyaeleza hayo wakati wa mahafali ya 10 ya skuli ya maandalizi Star Nursery school iliyopo kichungwa Wilaya ya Chake Chake, pamoja na kuzungumza wazazi na walezi wa watoto.
Alisema iwapo wazazi watashindwa kutekeleza kwa vitendo mikataba wanayopewa skuli, skuli hizo zitakosa maendeleo ikizingatiwa hazina bajeti wala ruzuku kutoka serikalini.
“Nivizuri tukahakikisha tunatekeleza kwa vitendo mikataba yote, ikiwemo kulipa malipo ya wanafunzi kwani malipo hayo ndio yanayopelekea skuli kujiendesha”alisema.
Akizungumzia mikakati ya serikali ya awamu ya nane, alisema serikali hiyo imedhamiria kwa dhati kusimamia suala la elimu, kwa kuanza kupitia mitaala ya elimu msingi na maandalizi pamoja na sera, ambayo itakapomaliza itapunguza wingi wa masomo kwa wanafunzi.
Alisema baraza la Mji linajukumu la kusimamia elimu ya sngi, afya na kilimo, baada ya kugatuliwa kutoka katika taasisi zao sasa zimeshuhwa chini katika mabaraza na halmashauri.
“Rais Dk Mwinyi amesema kutakua na mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu, dhamira hii inaweza kufikiwa iwapo tutakua kitu kimoja na kuipa mikakati madhubuti sekta ya elimu”alisema.
Aidha alisema Rais ameshaamua kuibadilisha sekta ya elimu, hivyo wananchi na wazazi wanapaswa kuongeza nguvu katika masuala ya elimu kwa kuhakikisha wanafuatilia kwa vitendo mienendo ya watoto wao.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa skuli ya Star Nursery school Bimoza, alisema skuli hiyo ilianza kazi 2001 hadi sasa inafikisha miaka 10, huku akiwashukuru wadau wa elimu na taasisi nyengine kwa kuunga mkono skuli hiyo kufikia malengo yao.
Alidha aliishukuru serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kufanya kazi zao kwa kuwepa mwelekeo kupitia taasisi zake ikiwemo wizara ya elimu.
Akizungumzia changamoto bimoza alisema kubwa ni suala la mapilipo kwa wazazi bado hawajalitimia mkazo, kwani kuna wanafunzi wanamaliza skuli lakini wazazi wao bado wanadaiwa skuli.
“Ndugu wazazi tambueni kuwa fedha munazolipa, ndio zinatumika kwa uwendeleshaji wa skuli yetu sisi hatuna ruzuku yoyote kutoka skuli, fedha hizo hizo tunatumia kulipia mishahara walimu”alisema.
Aidha Bimoza aliomba kupatiwa fedha za uji kwa skuli yao, kama zilivyo kwa skuli za serikali zinazvyopatiwa kwa wanafunzi wa maandalizi.
Jumla ya wanafunzi 80 wamehitimu katika skuli hiyo ya Star Nursery school,