Thursday, October 31

NMB yakutana na wakulima wa mwani na chumvi.

 

Benk ya NMB Kisiwani Pemba, imekutana na wakulima wa zao la Mwani na Chumvi katika shehia ya Kiungoni na Mjini Kiuyu, kwa lengo la kujua changamoto zinazo wakabili wa kulima hao.

Wakizungumza na wakulima hao kwa nyakati tafuti, uongozi wa NMB umesema lengo ni kujuwa changamoto zinazowakabili na kuona jinsi gani wanaweza kuwasaidia.

Meneja Mwandamizi kutoka idara ya kilimo na biashara Bank ya NMB Tanzania Wogofya Mfalamagoha, alisema NMB ni miongozi mwa mabenk yaliyopiga hatua kubwa Tanzania, huku ikiwa mstari wambele kusaidia katika sekta ya kilimo, uvuvi.

Alisema katika kuelekeza nguvu zao kama benk, imeakua kuanza na wakulima wa mwani na chumvi, kwani ndio wakulima wanaopata tabu kutokana na vilimo vyao.

Wogofya alisema wakulima wa mwani na chumvi huwapatia vipaombele zaidi, kwa kuwasiaidia vifaa, kujuwa soko lao likowapi, hata mazingira ya ukulima wenyewe na uwanikaji wake.

“Sisi tumekuja kujua changamoto zinazowakabili wakulima hawa, kuona wapi kama benk tunaweza kutia mkono wetu, ila vizuri katika kusaidia wakawa na vikundi vya ushirika wao hapo itakuwa rahisi kwetu”alisema.

Hata hivyo aliwataka wakulima hao kutambua kuwa, NMB inatoa mikopo hata ya kilimo kwa lengo la kuwasaidia wakulima wadogo wadogo, pamoja na kutoa bima ya kilimo pale wakulima wanapopata na matatizo ikiwemo mazo kuharibiwa na mabadiliko ya hali ya hema.

Alifahamisha kuwa katika kufikia malengo hayo kwanza wataanza na kutoa mafunzo mbali mbali, juu ya kilimo na uvuvi katika kuwafundisha utafutaji wa masoko na kulima kilimo cha biashara.

Kwa Upande wake meneja wa NMB Tawi la Pemba Hamada Msafiri, alisema NMB ni miongoni mwa benk inayohusika na masuala mbali mbali, ikiwemo kuharakisha maendeleo ya nchi kupitia kwa wakulima wadogo wadogo.

Alisema kwa sasa NMB inamatawi zaidi ya 200 Tanzania nzima, huku akisikitishwa na wakulima wengi sasa kulima kimazowea mtu mmoja mmoja, badala yake kulima kisasa kwa vikundi pamoja na kuondokana na uzalishaji wa mazao kwa matumizi badala yake kuzalisha mazao ya biashara.

Sheha wa shehia ya Kiungoni Omar Khamis Othaman, alisem aujio wabenk hiyo kijijini kwao, itakuwa ni faraja kubwa kwani wakulima wa mwani na Chumvi wataweza kunufaika kwa kusogeza maendeleo kwa wananchi.

Abdalla Suleiman Seif mkulima wa Chumvi kutoka Madenjani, alisema Kisiwa cha Pemba kimejaaliwa kuw ana wakulima wengi wa chumvi, wanashindwa kujitokea kutokana na kua na hofu ya kurudishwa nyuma kusonga mbele.

Alisema kama watasaidiwa vitendea kazi basi wanauwezo wakuzalisha chumvi kwa mwaka mzima bila ya kutetereka, kutokana uwezo mkubwalionao.

Iddi Ali Hamad mkulima wa Chumvi kutoka Shengejuu, alisema changamoto kubwa inayowakabili ni ukosefu wa soko, barabara na viwanda vyao kuwa vidogo vya uzalishaji wa bidhaa hiyo.

“mgodi wangu wa chumvi naweza kuzalisha paketi elfu 15 kwa msimu mmoj,a lakini sasa kutokana na kutokuwepo kwa soko, paketi elfu 3000 hazizidi ninazozalisha”alisema.

Naye Mtumwa Salum Hamada kutoka Mkulima wa mwani kutoka Shengejuu, alisema changamoto kubw ainayowakabili ni upatikanaji wa soko, bado bei ya mwani ni ndogo kilo shilingi 600, ukosefu wavitendea kazi ikiwemo kamba, viatu na vihori vya kubeba mwani.