MBUNGE wa Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete Hamad Hassan Chande, amekabidhi vifaa mbali mbali vya michezo kwa vilabu 19 vinavyoshiriki ligi madaraja mbali mbali Kisiwani Pemba.
Msaada huo uliotolewa ni seti zajezi na mipira kwa timu hizo 19 za kwanza zilizomo ndani ya jimbo hilo, huku timu zilizobakia zikitarajiwa kupatiwa wiki ijayo.
Akikamibidhi msaada huo Mbunge Huyo wa Jimbo la Kojani, alisema lengo ni kuhakikisha anainua viwango vya michezo kwa vijana wa waliomo ndani ya jimbo hilo pamoja na majimbo ya jirani.
Alisema kwa sasa amebakiwa na madeni mawili katika sekta ya michezo, kwa kubakia viwanja vitatu ambavyo hajavitengeneza na tayari vitatu alishavitengeneza kwa awamu ya kwanza.
Alisema deni la pili ni timu mbili kuwakabidhi posi za magoli, kwa ajili ya kuweka katika viwanja vyao huku akivitaka vilabu kujiandaa na ligi maalumu ya jimbo la Kojani.
“Hapa kila timu itupatie kiongozi wake, tukutane na tuandae ligi ya jimbo ambayo itaweza kushirikia vilabu vyte vya jimbo, lengo ni kuinua vipaji vya wachezaji katika jimbo letu”alisema.
Alisema mashindano hayo yatakapomalizika yataweza kutoa timu moja itakayoweza kushindana na timu yoyote kutoka nje ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Katibu wa timu ya Madenjani City Suleiman Ali Suleiman, alimshukuru mbunge huyo, kwani timu yao ilikuwa na upungufu wa vifaa vya michezo na vitaweza kuwasaidia sana.
Alisema changamoto kubwa ligi kukosa mdhamini, hivyo ali mtaka mbunge huyo kushirikiana na wabunge wenzao, kuhakikisha wanaipatia ufadhili dili daraja la pili wilaya ya Wete.
Naye Said Salum Mgau kiongozi wa timu ya Kajima FC, kupatiwa vifaa hivyo ni moja ya motisha kwa wachezaji sasa wachezaji watacheza mpira kwa bidii, huku akimtaka mbunge huyo kuwa karibu na wachezaji.