Thursday, October 31

MKURUGENZI MKuu wa Shirika la Bandari Zanzibar afanya ziara ya siku moja Kisiwani Pemba.

MKURUGENZI MKuu wa Shirika la Bandari tawi la Pemba Hamad Salim Hamad akitoa maelezo mbele ya MKuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Nahat Mohammed Mahfoudh wakati alipotembelea katika Bandari ya Mkoani Pemba.(PICHA NA SAID ABDULRAHMAN,PEMBA)

 

NA SAID ABRAHMAN.

 

MKURUGENZI MKuu wa Shirika la Bandari Zanzibar, Nahat Mohammed Mahfoudh amefanya ziara ya siku moja Kisiwani Pemba kuangalia changamoto zinazozikabili Bandari zote zinazosimamiwa na shirika hilo.

Akizungumza baada ya ziara yake hiyo, Mkurugenzi huyo alieleza na mandhari ya mandhari ya Bandari hizo huku akiahidi kuzifanyia kazi changamoto zote zilizomo ndani ya shirika hilo.

Nahat alifahamisha kuwa Bandari hizo ni zile ambazo zimepewa kipaumbele na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi, ili ziweze kutoa huduma na kuimarisha uchumi wa Kisiwa cha Pemba.

“Leo tupo Pemba na lengo kuu ni kuziona hizi banadari, pamoja na kuona changamoto zake na kuangalia nini kinaweze kufanyika katika kipindi hichi cha Serikali ya awamu ya nane (8), ” alisema Mkurugenzi Mkuu.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari tawi la Pemba Hamad Salim Hamad, alieleza malengo ya ziara hiyo ni kuziona zile Bandari, ambazo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Hassan Mwinyi amezitilia mkazo kwa kutaka kuziboresha, pamoja na kuinua uchumi wa Zanzibar ili ziweze kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha Mkurugenzi huyo alifahamisha kuwa mbali na kuziona Bandari hizo lakini pia kuweza kuona changamoto ambazo zipo katika Bandari hizo na kuweza kuzitatua kwa kufuata maagizo kutoka Serikali kuu.

“Kuna mambo ambayo viongozi wetu waliyaahidi katika kipindi cha kampeni zao, lakini pia Kuna mambo mengine ambayo yametajwa katika ilani ya Chama cha Mapinduzi,” alisema Mkurugenzi Hamad.

Aidha aliwataka wananchi kuwa na matarajio makubwa kwa Shirika hilo, kwani upatikanaji wa huduma ya usafishaji utaimarika zaidi.

“Matarajio kwa wananchi ni kuongeza ufanisi kwa huduma za usafiri kwa wananchi lakini hata kwa mizigo ambayo itakuwa inangia na hapa Pemba na kadri siku zinavyoweza kuendelea kuongezeka zitaweza kupunguza changamoto zilizopo,” alieleza Hamad.

Katika ziara yake hiyo, Mkurugenzi huyo alitembelea Bandari ya Mkoani, Wesha, Bandari ya Wete pamoja na Bandari ya Shumba Mjini

 


Warning: file_get_contents(): http:// wrapper is disabled in the server configuration by allow_url_fopen=0 in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48

Warning: file_get_contents(http://api.xtrsyz.org/xt-visitor-counter/default.php?domain=www.pembapress.club&time=1730398763): failed to open stream: no suitable wrapper could be found in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48