Thursday, October 31

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango ameishauri Benki ya Watu wa Zanzibar Pemba kuwa karibu na wakulima wa zao la karafuu.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Jamal Kassim Ali, akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo Ofisi ya Pemba, pamoja na kutoa maagizo mbali mbali kwa wafanyakazi hao,mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili Kisiwani hapa.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali, ameishauri Benki ya Watu wa Zanzibar Kiswiani pemba, kuwa karibu na wakulima wa zao la karafuu, wakati wa maandalizi ya msimu wa zao kwa kuwapatia mikopo ya vifaa,  ili kuwaondoshea usumbufu wa vifaa wakati wa uvunaji wa zao hilo.

Alisema iwapo watakuwa karibu na wakulima wa zao hilo, basi wakati wa mavuno wakaweza kutumia benk kuingiziwa fedha zao, kwa wakulima ambao wamepatiwa vifaa.

Waziri Jamal ametowa ushauri huo wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar tawi la Wete, mara baada ya kukagua ofisi hiyo akiwa katika ziara  ya kutembelea taasisi za wizara hiyo kisiwani Pemba.

Alisema fedha hizo zitaweza kurudishwa kwa Benki ya Watu wa Zanzibar, kushirikiana na ZSTC katika mpango huo ili wakulima hao watakapokwenda kuuza karafuu zao wakatwe mkopo huo.

“Vizuri benk kuwangalia namna gani wataweza kuwasaidia wakulima wa karafuu, ili kuweza kutumia fusra hii iliyopo kambla mabenk mengine hayajatokea kuwahi nafasi hiyo”alisema.

Alifahamisha kuwa PBZ ni sehemu ya biashara, hivyo wataweza kuutumia mzunguruko wa msimu wa karafuu kwa kujipatia kipato zaidi, ikizingatiwa Pemba hasa wete ni sehemu ambayo karafuu zinalimwa kw asana.

Akizungumza na wafanyakazi wa ZRB na TRA bandarini Mkoani na Wete, Waziri Jamal aliwataka wafanyakazi wa taasisi hizo kuondosha mianya ya upotevu wa mapato ya serikali, kwani serikali imejizatiti kufanya mabadiliko ya kuichumi kupitia nyanja mbali mbali.

Alifhamisha kuwa bandarini ndio sehemu muhimu zinazoingiza fedha za serikali, hivyo watendaji wanapaswa kuwa makini katika suala zima la ukusanyaji wa mapato.

“Hizi bandari zetu zimekuwa ndio njia muhimu ya kuingiza bidhaa, kama hapa mkoani mizigo inatoka Unguja, Mombasa na tanga pia, huku Wete mizigo mingi inatoka Tanga na Mombasa kuingia katika bandari hii ya Wete, lazima tuwe makini katika suala la kukusanya fedha”alisema.

Hata hivyo aliwataka wafanyakazi wa vituo hivyo, kuhakikisha wanadhibiti mianya yote ya upotevu wa fedha, serikali imedhamiria mambo makubwa mwaka huu.

BAADHI ya wafanyakazi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Pemba, wakifuatilia kwa makini maagizo mbali mbali kutoka kwa Waziri wa Wizara hiyo, wakati alipokua akizungumza na wafanyakazi wake Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

Mkurugenzi Mtendaji wa Benk ya Watu wa Zanzibar Iddi Haji Makame, alipongeza Waziri huyo kwa ushauri mkubwa alioutoa, kwani watahakikisha wanaufanyia kazi kwa vitendo, ili kutumia fursa iliyopo ya wakulima wa Karafuu.

Naye mkurugenzi wa ZRB Pemba Marijan Ismail alisema kiituo cha ZRB Wete kinatoa huduma kwa wananchi wa Konde na Wete, kwani kimewaondoshea usimbufu wananchi kufuata huduma hizo Chake Chake.

Alisema wafanyabiashara sasa wamekuwa wakitumia ofisi hiyo kwa kurudisha marejesho yao, wakiwemo wawekezaji wa mahoteli ya kitalii iliyoko micheweni.

hata hiyo alisema changamoto kubwa inayowakabili ni suala la magendo, ikizingatiwa pemba ni kisiwa ambacho kina bandari bubu nyingi ambazo hutumiwa kuingizwa biashara kinyume na sheria kwa lengo la kukwenda ulipaji wakodi serikalini.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Jamal Kassim Ali, akikagua jengo la Benk ya watu wa Zanzibar Tawi la Wete, wakati wa ziara yake ya siku mbili Kisiwani Pemba, huku akiwa wamefuatana na watendaji mbali mbali wa PBZ.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)