Thursday, October 31

Wahitimu 51 wa Skuli ya Ng’ambwa watunukiwa vyeti.

ALIYEKUWA afisa Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba Fatma Hamad Rajab, akimkabidhi cheti mmoja ya wahitimu a mahafali ya 13 ya kidato cha Nne skuli ya Ng’ambwa Abdull-shakur Abdalla Mohamed.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WAZAZI na Walezi wameshauriwa kutumia lugha nzuri kwa walimu wakati wanapotakiw akufika skuli, pamoja na kufuatilia mienendo ya watoto wao kielimu.

Ushauri huyo umetolewa na aliyekuwa Afisa Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni sanaa na Michezo Pemba Fatma Hamad Rajab, wakati alipokuwa akizungumza na wazazi, walezi na wanafunzi wakati wa mahafali ya 13 ya skuli ya Sekondari Ng’ambwa Wilaya ya Chake Chake.

Alisema mashirikianao mazuri baina ya wazazi, walezi na walimu ni jambo zuri linalopelekea wanafunzi kusoma kwa bidii, kwani kila mmoja anakuwa tayari kusimamia suala la elimu.

Alifahamisha kwamba wazazi wanaposhindwa kufuatilia mienendo ya watoto wao, basi watoto hao hupelekea kufanya vibaya katika mitihamnbi yao, pamoja na kuwa na maendeleo mabovu ya elimu skulini hapo.

Aidha aliwataka wanafunzi hao wanaomaliza masomo yao, kuhakikisha wanajitambua na kuishi na jamii vizuri kwa kuachana na makundi na badala yake kuingia katika vyuo vya amali.

“Katika suala la mkitihani kuna watakao fauli, watakaopata vyeti lakini chamsingi vipo vyuo vya amali vizuri kuvitumia vyuo hivyo kuliko kuliko muda mwingi kuutumia kwenye vikundi vionu,”alisema.

Aidha mhamini huyo aliahidi kuchangia skuli hiyo shilingi laki 5, pamoja na wanafunzi watakaofanya vizuri atawazawadia kwa hali na mali ili kufikia malengo yao”alisema.

Mwalimu mkuu wa Skuli hiyo mzuri Salim Mohamed, aliwataka wanafunzi hao wanaomaliza masomo yao, kukaa vyema na jamii pamoja na kutokuwakwaza wazazi na kuwa watu wema kwa sasa.

Alisema katika jamii  watakumbana na vishawishi vingi, hivyo aliwasihi kutokukubali kushawishika kwani bado wazazi wao wanaimani na vijana wao.

Hata hivyo aliwataka wanafunzi waliobakia kuzingatia muda wa masomo, huku akiwataka wazazi kuzidisha mashirikiano ili wanafunzi waliopo waweze kufikia malengo yao, pamoja na malengo ya skuli ikiwemo kupasishwa wanafunzi wote.

Akisoma risala ya wanafunzi mwanafunzi Raiyan Jailani, alisema skuli hiyo bado inakabiliw ana changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa vifaa vya sayansi nkulini hapo, uhaba wa chakula kwa wanafunzi wanakuwepo kambini wakijiandaa na mitihani.

Alisema changamoto nyengine ni kuchelewa kumaliziwa kwa majengo yao ambayo yamefikia hatua ya kuezekwa, huku wakiwaomba wadau mbali mbali kijitokeza kusaidia nguvu kazi za wazee hao.

Skuli ya Ng’ambwa Sekondari ni miongoni mwa skuli konge zilizobakia katika wilaya ya chake chake, ambapo ilianishwa 1948, huku ikiwa imekaliwa na walimu wasiopungua wakuu 30 tokea kuanzishwa kwake, ambapo jumla ya wahitimu 52 wanatuki vyeti vyao vya kumalizia masomo yao.

ALIYEKUWA afisa Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba Fatma Hamad Rajab, akipata maelezo juu ya mfumo wa umeme na kupatikana kwa mwanga wake, kutoka kwa mmoja ya wahitibu wa kidato cha nne kutoka skuli ya Ng’ambwa Sekondari Shauri Khamis Hamad, wakati alipokagua kazi za mikono kwa wahitimu hao.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)