Friday, November 1

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo hii leo Visiwani Zanzibar, Waziri Mwalimu yuko Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha

Na Lulu Musa

Waziri Ummy Mwalimu amefanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharrif Hamad Chukwani Zanzibar.

Mhe. Hamad amesisitiza umuhimu wa Wizara zenye hoja za Muungano kukutana na kutafuta suluhu ya mapema na kuhamasisha  Wizara zisizo na hoja kukutana pia kwa lengo la kudumisha undugu baina ya  Tanzania bara na Tanzania Zanzibar.

“Nashauri na kusisitiza Wizara zinazoshabihiana zikutane na kuhakikisha hoja zinazopatiwa ufumbuzi zitekelezwe ipasavyo” alisisitiza Maalimu Seif Sharif Hamad.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo baina yao hii leo Visiwani Zanzibar.

Waziri Ummy Mwalimu yuko visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na hapo kesho atatembelea miradi ya Muungano inayotekelezwa pande zote mbili.