Wakulima wa kilimo cha muhogo na viazi katika Shehiya ya Mbuzini Chake Chake wameanza kunufaika na mbegu za muhogo aina ya kizimbani pamoja na viazi mayai ambazo zimefanyiwa utafiti na Idara ya Utafiti Kisiwani Pemba,
Akizungumza na Waandishi wa habari wakati walipokuwa katika ziara ya kuwatembelea wakulima hao ili kuona matokeo ya utafiti wa mbegu hizo Mmoja kati ya wakulima hao Bibi Fatma Bakar Hamad amesema kwa kipindi cha miaka minne sasa tokea kuanza kupanda mbegu hizo amekuwa akipata mazao hayo kwa wingi na kuleta tofauti kubwa katika miaka yote alioanza kulima kilimo hicho.
Naye Mkuu wa utafiti wa zari Pemba ,Khatib Bakar Haji amesema baada ya utafiti huo mbegu hizo zimebainika kuwa na sifa ya kustahamili ukame lakini pia zinatoa mazao kwa wingi na kupunguza changamoto ya uhaba wa chakula kwa wakulima hao.
Kwa upande wake Kamishna Mkuu Idara nya Utafiti Zanzibar Bibi Afua Mohammed Khalfan amewataka Waandishi wa habari kuwaelimishwa wananchi juu ya kutumia mbegu hizo ambazo tayari zimefanyiwa utafiti na kuonesha tija kubwa kwa wakulima.
Angalia video