Waandishi wa habari Kisiwani Pemba wametakiwa kujikita katika kuandika habari za mambo yaliyofanyiwa utafiti ili jamii iweze kufahamu matokeo ya tafiti mbali mbali zinazofanywa nchini kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.
Akiwasilisha mada juu ya mbinu za Uandishi wa habari za Utafiti Dk. Ali Uki huko katika ukumbi wa maabara ya afya ya jamii Wawi amesema katika nchi huwa kuna fanywa tafiti mbali mbali lakini matokeo yake hayawafikii wananchi.
Amesema ili taarifa hizo ziweze kuifikia jamii ni lazima waandishi wa habari wawe karibu na watafiti ili waweze kupata habari hizo na kuzifikisha kwa jamii kwa lugha ambayo wataweza kuifahamu kwa urahisi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya menejimenti ya maarifa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dk. Bunini Manyilizu amesema matokeo ya tafiti hizo ndio itakayopelekea kuleta mabadiliko ya maendeleo kwa jamii.
Mafunzo hayo ya siku tatu juu ya uandishi wa habari za Kiutafiti yamewashirikisha waandishi wa Habari na watafiti Kisiwani Pemba ,ambapo yameendeshwa na Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu na tayari mafunzo kama hayo yameshafanyika katika mikoa mbali mbali ya Tanzania.
Angalia video