Thursday, January 30

Uwanja wa Nyungwinyungwi wafanyiwa matengenezo.

KIFAA maalumu kikiweka sawa uwanja wa michezo Ndugukitu unaotumika na Timu ya Machomanne United, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi za viongozi wa Jimbo la Wawi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

VIONGOZI wa Jimbo la Wawi wamesema wanakusudia kuleta mabadiliko makubwa katika michezo, kwa kutekeleza sheria 17 za mpira wa miguu duniani, ikiwemo kuimarisha miundombinu ya viwanja na kuweza kutumika muda wote.

Kauli hiyo imetolewa na mbunge wajimbo la Wawi Khamis Kassim Ali, mara baada ya kushuhudia zeozi la ufanyaji wa matengenezo uwanja wa Nyungwinyungwi shehia ya Mkoroshoni.

Alisema kiwanja hicho ni cha tatu kutengenezwa kwa kukiweka sana kufikia mita 100, magoli ya kisasa na nyavu kwa lengo la kuondosha usumbufu kwa wana michezo.

                                                         MBUNGE wa Jimbo la Wawi Khamis Kassim Ali

Naye mwakilishi wajimbo hilo Bakar Hamad Bakar, alisema wanakusudia kuinua viwango vya michezo katika jimbo hilo, kwa kuzisajili timu na kuweka miundombinu sahihi ya viwanja vya michezo.

Alisema utekelezaji huo unatokana na ilani ya CCM, kwani tayari walishavipatia fedha za usajili timu, pamoja na vifaa vya michezo.

“Katika jimbo lao limekuwa na vilabu vingi vikubwa ambavo vinatajika, lakini havionekani umuhimu wake kutokana na kuwa na miundombinu mibovu kwa muda mrefu ya viwanja”alisema.

Mwakilishi wa jimbo la wawi Bakar Hamad Bakar

Kwa upande wake katibu wa uwanja huo Abdull, alisema wameshindwa kuendelea michezo yao kwani uwanja hupo huutumia katika siku za jua tu, kipindi cha mvua hua ni changamoto kubwa kutokana na kukaa kwa maji.

Viwanja ambavyo mpaka sasa vimeshafanyiwa matengenezo na viongozi wajimbo la Wawi, ni Ndugukitu unaotumiwa na timu ya Machomanne United, Ngengere unaotumiwa na timu ya Hard Rock pamoja na Nyungwinyungwi mkoroshoni.