Sunday, March 16

WAZAZI elekezenikuekeza nguvu zaidi katika suala zima la elimu kwa watoto.

MWAKILISHI wa Jimbo la Wawi Bakar Hamad Bakar, akizungumza na wazazi, walimu na wanafunzi wakati wa mahafali ya kwanza ya skuli ya Al-jitihad Nnisai Islamiya iliyopo Kichungwani Wilaya ya Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WAZAZI wametakiwa kuekeza nguvu zaidi katika suala zima la elimu kwa watoto wao, kwani bila ya elimu hakuna kitu chochote kitakachoweza kuwasaidia.

Hayo yameelezwa na mwakilishi wajimbo la Wawi Bakar Hamad Bakar, wakati alipokua akizungumza na wazazi, walimu na wanafunzi katika mahafali ya kwanza ya skuli ya Al-jitihad Nnisai Islamiya Iliyopo Kichangani Wilaya ya Chake Chake.

Alisema katika miaka ya hivi karibuni wazazi wamejikita zaidi kuchangia mambo ya dunia, kuliko kuchangia malipo ya watoto wao skuli, pamoja na kushindwa kulipa kipaombele suala la elimu.

Alifahamisha kuwa elimu ndio msingi wa maisha ya mtoto, huku serikali ikijitahiti kutekeleza sera ya elimu bure, ili kuwapa nafasi watoto kusoma zaidi.

“Leo mzazi yuko tayari kuchagua harusi na maholi hata 10, lakini suala la kuchagia au kulipia ada mtoto wake skuli ni tatizo na kubwa kwake inakuwa”alisema.

“Jamani tutambue kuwa watoto wetu nao wanajisikia tabu ikiwa anadaiwa ada skuli, ada hizo hizo ndio zinazolipiwa walimu mishahara vizuri tukajitahidi kulipa”alisema.

Aidha Mwakilishi huyo aliwataka wazazi kutimiza wajibu wao katika kuwalea watoto wao katika maadili mema, pamoja na kutumia lugha nzuri wanapokua majumbani.

Alisema watoto wamekuwa wepesi kuiga mambo mbali, hivyo wazazi hawana budi kuacha kutumia lugha mbaya wanapokuwepo watoto au kuwaita majina ambayo hayafai kuitwa binaadamu.

“Lazima tuwe makini tunapokuwa na watoto wetu, tujaribu kutumia lugha nzuri hata sisi wazazi, hatupaswi kugombana wanapokuwepo watoto wetu, kwani nao wanaweza kuiga tabia hizo hapo baadae”alisema.

Kwa upande wake mwalimu Mkuu wa skuli ya Al-jitihad Nnisai Islamiya Iliyopo Kichangani, Ali Mohamed Salim alipongeza wizara ya elimu kuwasaidia vitambu, ambapo alifahamisha kuwa skuli hiyo bado inaendeshwa kwa michango ya wanafunzi.

Hata hivyo alisema licha skuli hiyo kukabiliwa na changamoto mbali mbali, ikiwemo ukosefu wa Komputa za kufundishia somo la IT skulini hapo.

Akisoma risala ya walimu ya katika mahafali hayo Mwanafunzi Faridi Hamad Seif mhitumu STD 6, alisema lengo kuu ni kuongeza madarasa ya msingi,taaluma iltolewayo ni sawa na ile ya mtaala wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema mafunzo ya dini ya kiislamu yamepewa kipawa mbele ndani ya sku hiyo, huku changamoto kubwa inayowakabili mishahara ya walimu kuwa kiwango kidogo , ukosefu wavifaa mbali mbali ikiwemo vifaa vya michezo, vitendea kazi, vikalio na usafiri.