Idara ya Takwimu za Kijamii Zanzibar imekuwa ikifanya Utafiti juu ya masuala ya Jinsia,mila,desturi,sheria na tamaduni Zanzibar ili kuibua changamoto mbali mbali zinazoikabili jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vilivyopo Kisiwani Pemba Afisa kutoka Idara ya Takwimu Pemba Nachia Ali Salim amesema ndani ya jamii kuna changamoto mbali mbali zinazoleta tofauti za kijinsia lakini bado taarifa sahihi juu ya tofauti hizo hazijajulikana.
Kwa Upande wake Mdhibiti viwango kutoka Ofisi ya Takwimu Hamad Khamis Rashid amesema katika utafiti huo wanaangalia kwa kina juu ya sababu ya tofauti hizo.
Akitoa Ufafanuzi juu ya Utafiti huo Mkuu wa Idara ya Takwimu za Kijamii Zanzibar Khadija Khamis amesema wanajaribu kuaangalia kwa kina jinsi jamii inavyochukulia Usawa wa kijinsia kati ya Mwanamke na Mwanamme katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku, kwani mara nyingi imekuwa ikionesha kwamba bado kunauwelewa mdogo juu ya usawa wa kijinsia miongoni mwa jamii.
Utafiti huo ulianza rasmi tarehe 10 Disember , 2020 na kwamba unatarajiwa kukamilika tarehe 11 january,2021 ambapo unaendeshwa kwa mashirikiano kati ya OCGS,NBS,OECD na shirika la Maendeleo ya wanawake la Umoja wa Mataifa UN WOMEN.
ANGALIA VIDEO HAPA.