NA ABDI SULEIMAN.
VIJANA kisiwani Pemba wametakia kutambua kuwa suala la uzalendo katika nchi, ni kitu cha kukilinda na kujitolea kwa 100% ili kufikia malengo ya serikali ya awamu ya nane yaliyokusudiwa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa baraza la Mji Chake Chake Salma Abuu Hamad, wakati alipokua akizindua zoezi la ufanyaji usafi katika Hospitali ya Vitongoji, lililoendeshwa na umoja wa Vijana wa UVCCM Wilaya ya Chake Chake, ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Alisema suala la usafi ni kitu muhimu katika maisha ya mwanaadamu, ndio maana Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wabaraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwnyi, amekua akilipigia kelele kuufanya mji wa Zanzibar kua msafi muda wote.
Aidha aliwashukuru vijana hao wa UVCCM kwa kufanya kazi hiyo ya kiunganwa, kwani ni suala la kujitolea na kuona wanayaenzi Mapinduzi ya 1964, kwa kufanya kazi za kizalendo kusafisha Hospitali ya Vitongoji.
“Usafi ni afya lazima tuhakikishe mazingira yetu yanakuwa mazuri, kwani tunaondoa maradhi mbali mbali nyemelezi, ikiwemo Kipindupindu, maradhi ya kuharisha hata malaria hususana kipindi hiki cha mvua”alisema.
Aidha alisema katika kipindi hiki wananchi wanapaswa kusafisha vichaka ambavyo vilivyopo kwenye maeneo yao, kwa lengo la kujiepusha na ugonjwa wa malaria, huku akisema hata wagonjwa waliopo spitali wataona na kufarahia Mapinduzi.
Hata hivyo alisema usala la usafi ni moja ya majukumu yao mabaraza la Miji, wanahakikisha suala la usafi wanalifanyia kazi kwa vitendo. hata Rais Dk.Hussein Mwinyi katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ,adhma yake moja ni kuhakikisha miji ya Zanzibar inakuwa safi.
Hata hivyo aliwapongeza Vijana wa UVCCM Chake Chake, kuadhimisha Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Vitongoji, kwani ni jambo la kupigia mfano kwa umuzi huo wa Vijana.
Daktari dhamana wa Hospitali ya Vitongoji Sharif Hamad Khatib, aliwashukuru vijana hao wa UVCCM kwa kuamua kufanya usafi katika hospitali hiyo, kwani ni moja ya sehemu muhimu kwa jamii pamoja na wagonjwa.
Alisema Mapinduzi ya mwaka 1964 yameweza kuwakombo wazanzibari kutoka kwa wakoloni, huku Mwasisi wa Mapinduzi hayo Mzee Karume aliasisi huduma za matibabu kuwa bure kwa wananchi wote.
Alifahamisha kuwa afya ni usafi na bila ya usafi hakuna afya, hivyo aliwataka vijana kuinga mfano wa Rais Dk.Mwinyi katika kauli mbiu yake ya kuhamasisha suala zima la usafi.
“Suala la usafi ni muhimu kwa jamii ujio wenu umeweza kutusaidia sana sisi, wafanyakazi kwani nguvu zenu zitapelekea hospitali yetu kungara leo”alisema.
KATIBU wa UVCCM Wilaya ya Chake Chake Thamrat Bakar Yussuf, alisema kuelekea maadhimisho ya Miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar vijana hawako nyuma wameamua kufanya usafi katika hospitali ya Vitongoji kwa wlengo la kuadhimisha Mapinduzi hayo.
Alisema katika kufanya usafi huo pia wamelazimika kutoa zawadi kwa watoto ambao ambao wamelazwa hospitalini hapo, kwani Mapinduzi hayo ndio yaliyopelekea kuwepo kwa uhuru mpaka sasa.
Kwa upande wao Vijana wa UVCCM Zuhra Sulieman, alisema tayari tokea kujiunga na UVCCM ameweza kunufaika na mambo mbali mbali, ikiwemo suala zima la elimu ya ujamaa, udhalilishaji, ushoni pamoja na kupatiwa ajira serikalini.
Hata hivyo aliwataka vijana wenzake kujiunga na kikundi chao hicho, kwani kuna fursa mbali mbali zinapatikana na kwa vijana ikiwemo kujengwa uzalendo na ukakamavu.