NA ABDI SULEIMAN.
WANANCHI wa Kijiji cha Limanda shehia ya Pujini Wilaya ya Chake Chake, wameliomba shirika la Umeme Zanzibar Tawi la Pemba kuwapatia umeme kwa njia ya Mkopo pale utakapofika kijijini kwao.
Wamesema kwa sasa wakotayari kuunganishiwa umeme huo kwa njia ya Mkopo pale tu utakapofika, licha ya kutolewa ahadi ya kijiji hicho kupelekewa umeme na Rais Mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya saba, tokea mwaka 2010 na 2015 wakati alipokua akiomba kura.
Wakizungumza na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo, kushuhudia zoezi la uwekaji wa Tansofa yenye uwezo wa 100KVA katika eneo la mradi wa Umwagiliaji Pujini Wilaya ya Chake Chake.
Mkubwa Massoud Juma alisema huduma hiyo ya umeme wameisubiri kwa muda mrefu, kwani utaweza kuwasaidia wananchi kwa shuhuli mbali mbali za kijamii, kilimo na ufugaji.
“Sisi huku watu wa pujini zaidi ni wakulima na wengi wetu tunavisima tunatumia kwa umwagiliaji maji shambani, sasa ukija umeme tutachana na utumiaji wa mafuta kwa janreta”alisema.
Alisema ahadi hiyo ya kuletwa umeme ilitolewa kwa vijiji vitatu Pujini, Mtimbu na limanda na Rais Mstaafu, sasa umeme ndio unatarajiwa kufika sasa.
Mbarouk Massoud Khamis alisema huduma ya umeme wanaitaka na wameisubiri kwa miaka mingi kijijini pao, kwa tawaweza kuitumia kwa shuhuli mbali mbali za kijamii na kimaendeleo.
Hata hivyo aliwataka wananchi wenzake kukaa tayari kuupokea umeme huo, pale utakapofika pamoja na kuzifanyia fitingi nyumba zao.
Kwa upande wake afisa Mawasiliano na huduma kwa wateja kutoka shirika la umeme ZECO Tawi la Pemba Haji Khatib Haji, lengo la kuwekaji wa Tansfoma hiyo ni kusogeza maendeleo katika kijiji mtimbu pamoja na eneo la uwekezaji mradi wa umwagiliaji.
Alisema tansfoma hiyo itaweza kusogeza huduma katika kijiji cha Limanda, ili wananchi waweze kunufaika na huduma ya umeme hiyo.
“Matarajio yetu baada ya kazi hii kumalizika wananchi wataweza kunufaika na mradi huo kwa shehia tatu, Matale, Dodo na Pujini na Tansfoma inauwezo kutoka huduma kwa kijiji na eneo la uwekeaji”alisema.
Hata hivyo alifahamisha kwamba kutokana na matumizi kuongezeka kwa wateja, lakini Tansofa hiyo itaweza kuhimili nguvu za wananchi na wawekezaji hao.
Kwa upande wake sheha wa shehia ya Pujini Khamis Uledi Kombo, kumalizika kwa kazi hiyo itaweza kusaidia juhudi mbali mbali za wananchi, sambamba na kulitaka ZECO kuongeza bidi katika kupeleka huduma ya umeme katika vijiji ambavyo bado huduma hiyo haijafika.
Kijiji cha limanda kina kaya 23 zenye wakaazi 75.