Fainali ya 15 ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuchezwa kesho Jumatano January 13, 2021 kati ya Yanga dhidi ya Simba saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Amaan.
Kuelekea katika Fainali hiyo, Abubakar Khatib (Kisandu) Muandishi wa Michezo Zanzibar kuna mambo muhimu unapaswa kuyafahamu kakuandalia:-
1. Yanga ndiyo timu pekee ambayo imeruhusu mabao machache (1) kuliko Simba ilokubali Nyavu zake kuguswa mara 2, hivyo Safu ya Ulinzi ya Yanga inayoongozwa na Mlinda Mlango Farouk Shikalo na Walinzi wake Kibwana Shomari, Adeyum Saleh, Abdalla Shaibu (Ninja) na Said Juma (Makapu) inaonekana ndio safu bora mpaka sasa Katika Mashindano hayo.
2. Simba wameingia fainali mara nyingi kuliko timu yoyote (na hii itakuwa mara 8) ambapo Yanga ndo kwanza hii fainali yao ya 3.
3.Simba na Yanga wamekutana mara 2 katika mashindano hayo na kesho itakuwa mara yao ya 3 ambapo mwaka 2011 walikutana fainali na Simba wakatwaa ubingwa baada ya kuwafunga Yanga 2-0 na mwaka 2017 walikutana tena kwenye nusu fainali dakika 90 mchezo ukamalizika kwa sare ya 0-0 na Simba ikashinda kwa Penalties 4-2.
5.Mashindano mwaka huu Simba imeshinda mabao mengi (mabao 7) ikiruhusu kufungwa mawili wakati Yanga wakishinda mabao 2 tu na kuruhusu kufungwa 1. (Safu bora ya Ushambuliaji ya Simba inakutana na safu bora ya Ulinzi ya Yanga)
6. Simba inaenda fainali bila ya kuwa na kocha wao mkuu ikiongozwa na msaidizi Suleiman Matola wakati Yanga imeenda fainali ikiongozwa na kocha wao mkuu Mburundi Cedric Kaze.
7. Miraji Athuman wa Simba ndiye kinara wa mabao hadi sasa akiwa na mabao 4 akifuatiwa na Meddie Kagere pia wa Simba mwenye magoli 2 na Steven Sey wa Namungo mabao 2.
8.Simba itacheza fainali ya Mapinduzi Cup miaka 3 mfululizo, ilicheza 2019 ikapoteza 2-1 mbele ya Azam, ikacheza 2020 ikafungwa 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar na itacheza mwaka huu 2021 kesho mbele ya Yanga, vipi Simba itaendelea kupoteza kwa mara 3 mfululizo?
9.Simba ambayo imecheza fainali 7 na hii ya kesho itakuwa ya 8, imeshinda 3 (mwaka 2008,2011 na 2015 na kupoteza 4 (Mwaka 2014,2017,2019 na 2020) wakati Yanga hii itakuwa fainali yao ya 3 kucheza pamoja na ya kesho, moja wameshinda 2-1 mbele ya Mtibwa Sugar mwaka 2007 na nyengine walifungwa na Simba 2-0 mwaka 2011, Je kesho ni Simba kubeba Kombe la 4 au Yanga kushinda kombe lake la 2?